Thursday, 29 October 2015

BREAKING NEWS: DKT JOHN POMBE MAGUFULI ASHINDA UCHAGUZI MKUU WA URAIS KWA KURA 8,882,935

 Dr. John Pombe Magufuli ametangazwa Rasmi na Jaji Luvuba kuwa ndiye Rais Mteule  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania




Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha CCM John Pombe Magufuli ndiye rais mteule wa taifa la Tanzania baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili.
Akitoa matokeo hayo mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa Magufuli alijipatia kura 8,882,935 ikiwa ni aslimia 58.46 huku mpinzani wake wa karibu Edward Lowassa wa chama cha Chadema akijipatia kura 6,072,848 ikiwa ni asilimia 39.97 ya kura zote.
Haya ndiyo matokeo kamili kama yalivyotangazwa na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania Jaji Mstaafu Damian Lubuva:
Matokeo ya uchaguzi wa urais Tanzania
JinaChamaKuraAsilimia
Anna MghwiraACT98,7630.65
Chifu YembaADC66,0490.43
John MagufuliCCM8,882,93558.46
Edward LowassaCHADEMA6,072,84839.97
Hashim SpundaCHAUMA49,2560.32
Janken KasambalaNRA8,0280.05
Macmillan LyimoTLP8,1980.05
Fahmi DovutwaUPDP7,7850.05
Awali kabla ya kutolewa kwa matokeo hayo Takriban vyama vitano kati ya vinane viliridhia kutia sahihi matokeo hayo ambayo tayari yamepingwa na chama rasmi cha upinzani CHADEMA.
Akivihutubia vyombo vya habari mgombea wa urais kupitia chama hicho Edward Lowassa amepinga matokeo yoyote ya uchaguzi huo na kujitangaza mshindi wa uchaguzi kwa kupata asilimia 62 ya kura zilizopigwa.
Lowassa amedai kwamba tume ya uchaguzi nchini humo imeshirikiana na chama tawala CCM kufanya udanganyifi katika shughuli hiyo.
Lakini akitoa matokeo hayo Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa baada ya kujumlisha matokeo yote ya urais katika uchaguzi huo,John Pombe Magufuli ndiye aliyeibuka mshindi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!