Saturday, 19 September 2015

MAKALA, Serikali ikomeshe mauaji ya raia kwenye mgodi wa Geita

 BAADHI ya wananchi wa mji wa Geita wakifanya maandamano kupinga kuuawa kwa mwanafunzi wa Darasa la sita Hoja Juma katika shule nya msingi Kivukoni,tukio ambalo linadaiwa kufanywa na Walinzi wa mgodi wa Geita(GGM).

MOJA ya uharibifu uliofanywa na waandamanaji wanaopinga unyanyasaji wanaodai kufanyiwa na Mgodi wa Geita,ambapo katika picha linaonekana Gari linalomilikiwa na Mgodi wa Geita likiteketea kwa moto baada ya kuchomwa na waandamanaji(Hawako pichani) (Picha na David Azaria)

Na David Azaria, Geita yetu 
MWISHONI mwa wiki iliyopita kundi kubwa la wananchi wa mji wa Geita waliandamana hadi katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Geita Manzie Mangochie, wakipinga kitendo cha kuuawa kwa mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi Kivukoni Mjini Geita kwa tuhuma za kukamatwa akiiba vyuma chakavu ndani ya Mgodi wa Geita. 
Kundi hilo hilo la wananchi lililokuwa na zaidi ya waandamanaji 500 pamoja na kupinga mauaji hayo walikataa kuuzika mwili wa marehemu ikiwa ni pamoja na kuutoa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitalin ya wilaya wakiutaka uongozi wa mgodi huo kushughulikia zoezi zima la Mazishi ya mwanafunzi huyo Hoja Juma. 
Katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu huyo wa wilaya Wananchi hao walidai wamechoshwa na vitendo vya mauaji ya raia ambavyo vimekuwa vikifanywa na walinzi wa mgodi wa Geita, ambao wamekuwa wakidaiwa kuingia ndani ya mgodi huo kwa ajili ya kuiba vyuma chakavu pamoja na miamba taka inayotupwa kama uchafu. 
Inaelezwa kwamba miamba taka hiyo yenye dhahabu kidogo huchukuliwa na wananchi hao na kuiponda kisha kuiosha na kupata dhahabu ambayo imekuwa ikiwasaidia kupata fedha na hivyo kuendesha maisha yao na hali hiyo imekuwa ikisababishwa na  ukosefu wa maeneo ya wachimbaji wadogo hali inayosababisha wawe watu wa kukimbia mara kwa mara. 
Mwanafunzi huyo alipigwa risasi na walinzi wa mgodi huo kwenye ubavu wake wa kulia na kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi wa Daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu, kifo cha marehemu kilisababishwa na kuvuja damu nyingi iliyosababishwa na kuharibiwa vibaya kwa mapafu yake na risasi. 
Wakizungumza na Kaimu Mkuu wa wilaya hiyo Moses Minga ambaye ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo walisema kumekuwepo na mauaji ya mara kwa mara ndani ya mgodi huo ambayo yamekuwa yakifanywa na walinzi wa mgodi huo na kutoa mfano kwamba katika eneo linalozunguka kiwanja cha Ndege cha Mgodi huo kumejaa harufu mbaya inayotokana na mizoga wananchi wanaouawa na walinzi hao. 
“Kuna ushahidi wa kutosha kwamba mauaji dhidi ya raia yamekithiri ndani ya mgodi wa Geita, mauaji yanayofanywa na walinzi wa Mgodi, ukipita kwenye eneo la uwanja wa Ndege wa Mgodi kumejaa harufu ya mizoga, sisi tunaingia huko mara kwa mara, lakini cha ajabu ni kwamba serikali imekaa kimya haijali maisha ya wananchi wake na hata wanaoingia humo mgodini hawapendi ni kwa sababu ya maisha magumu…..’’ alisema Muandamanaji mmoja mbele ya katibu Tawala aliyejitambulisha kwa jina la Valence Wilson. 
“Wanaoingia wote humo ndani ni kwa sababu ya shida zinazowakabili pamoja na kukosa maeneo ya uchimbaji, ndio maana wanaingia humo kuchukua magwangala kwa ajili ya kupata dhahabu ili waweze kumudu maisha yao,lakini kibaya zaidi wanakutana na vifo huko serikali ikiwa imekaa kimya bila kukemea ama kutafuta muafaka kwa pande zote mbili……’’ aliongeza. 
Mara kadhaa nimeandika makala katika Gazeti hili nikielezea kero kubwa wanayoipata wachimbaji wadogo wa wilaya ya Geita, maeneo yao mengi yamechukuliwa na wawekezaji wakubwa kama si kwa ajili ya shughuli za uchimbaji basi ni kwa ajili ya utafiti wa madini na kibaya zaidi hata watafiti wenyewe wamekuwa wakihodhi maeneo hayo kwa muda mrefu bila kuyaachia. 
Hakuna ubishi kwamba hatua waliyofikia wananchi wa wilaya ya Geita sasa ni kubwa na kama serikali ya wilaya na Mkoa haitakuwa makini katika kutatua mgogoro huo unaofuka moshi kwa sasa kuna siku ambayo kutakuja kuibuka vurugu kubwa ambazo zitasababisha maafa yasielezeka. 
Moja ya matokeo mabaya ya maandamano hayo ni ya hivi karibuni ambapo wachimbaji pamoja na wananchi wa mji wa Geita walifanya vurugu kubwa na kuharibu mali mbalimbali za raia ikiwa ni pamoja na kuchoma moto magari ya mgodi pamoja na kupasua vio vya magari ya raia wa kawaida. 
Suala la mahusiano mabaya kati ya wananchi wa wilaya hiyo pamoja na uongozi wa mgodi lipo tangu kuanzishwa mgodi huo miaka 10 iliyopita na sasa ‘Magwangala’ yamezidisha mahusiano hayo kuwa mabovu zaidi. 
Nasema hivyo kwa sababu katika kipindi chote hicho cha mahusiano mabovu kati ya wananchi na mgodi huo sio kwamba wananchi walikuwa hawalalamiki, walikuwa wanalalamika lakini chini kwa chini, ingawa kwa sasa chuki imekuwa ya hadharani na sio kificho tena. 
Kibaya zaidi ni kwamba wanaolalamika na kufanya vurugu ni vijana ambao ndio wanaaminika kujihusisha zaidi na shughuli za uchimbaji wa madini, lakini wakielezwa kwamba ndio pia wenye uwezo wa kuvuka milima na mabonde kabla ya kuingia na kutoka ndani ya mgodi huo huku ikielezwa kwamba maeneo wanayokwenda kuiba mawe ya dhahabu ni ya hatari kubwa. 
Kuna taarifa za baadhi ya wachimbaji hao kupoteza maisha kutokana na kutumbukia ndani ya mashimo hayo, huku wengine wakijikuta wakifukiwa ndani ya mashimo ya dhahabu na wenzao wakati wa kuiba mawe hayo ya dhahabu na wengine kutumbukia ndani ya maji na kupoteza maisha. 
Kibaya zaidi kwa sasa imefikia hatua ambapo sasa risasi za moto zinaanza kutumika dhidi ya raia kutoka kwa walinzi wa mgodi huo na kusababisha vifo,hii ni hali ya hatari ambayo inapaswa kuchukuliwa hatua za haraka tena za makusudi,vinginevyo ipo siku inakuja ambapo hali ya hewa itachafuka ambapo watu watatafuta milango ya kupitia lakini milango hiyo haitaonekana. 
Kuna haja kwa viongozi wa serikali katika Mkoa wa Geita wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula wakaketi chini na kuangali namna ya kulitafutia suala hili ufumbuzi wa kudumu.

No comments:

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!