Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mbogo Mfutakamba wakati akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye hafla ya kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mhandisi Stella Manyanya wakati akiwasili Mnazi Mmoja kwenye hafla maalumiliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi ya kumuaga Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Ilikuwa Siku ya furaha sana kwa wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi.
Kila mtu alichukua tukio lililomfurahisha kwa simu yake .
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi na kupokelewa na Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye Mhe. Sophia Mjema kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Injinia Stella Manyanya wakati akiwasili kwenye hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi
Wahandisi mbali mbali wa Wizara na wasiokuwa wa Wizara walijumuika pamoja kwenye hafla ya kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete
Wageni waalikwa kutoka taasisina mashirika mbali mbali walishiriki kikamilifu.
Wasanii wa JKT Mgulani wakionyesha wakisakata ngoma ya Msewe wakati wa sherehe za kumuaga Rais Jakaya Mrisho Kikwete zilizoandaliwa na Wizara ya Ujenzi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye hafla ya kumuaga Rais Jakaya Mrisho Kikwete iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi.
Rais Jakaya Kikwete akihutubia wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi wakati wa hafla maalum ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
Rais Jakaya Kikwete akikabidhiwa ufunguo wa trekta lake alilopewa zawadi kwenye hafla ya kumuaga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikweteakiwa kwenye picha ya pamoja na wahandisi wanaogombea ubunge kwenye majimbo mbali mbali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wanamuziki wa Bendi ya Sikinde ambao walikuwa wakitumbuiza kwenye hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi.
No comments:
Post a Comment