Sunday, 16 August 2015

STORI YA LEO:



Habarini za Jumapili.
Kadri siku zinavyokwenda na ugumu wa maisha unavyozidi, ndivyo hivyo hivyo kunavyoibuka kada mbalimbali za matapeli na mbinu mpya za utapeli wa kujipatia kipato!.


Mimi ni mkazi a Mbezi Juu, jirani na Hospitali ya Masana, leo nimetoka Church niko home naangalia marudio ya tamthilia ya Isidingo, nasikia mlio a boda boda imesimama nje, kisha mtu akabisha hodi, namtuma mtoto akafungue, akarudi kuniambia kuna mgeni ananiita nitoke nje, nikamtuma amkaribishe aingie ndani, jibu likaja mwambie tuu baba atoke, kuna jambo la dharura!.
Kiukweli hua sipendi kabisa kumiss hata scene moja ya tamthilia hii, ila kwa shingo upande nilitoka nikijiuliza ni nani na ana dharura gani?!, nikatoka kukutana na jamaa bonge la mtu, akanisalimia kwa kunichangamkia kama ananijua, akajitambulisha kwa kuniuliza "utakua umenisahau!, mimi ni Afande Juma, mkuu a kituo cha polisi cha Mbezi Juu, nimeishakusaidia sana kwenye issues za kipolisi, sema utakuwa umenisahau maana ni kipindi, ila pia naishi hapo jirani yako, mtaa wa nyuma, ukifika tuu pale na kuulizia Afande Juma, utanipata".
Akanieleza umepata na dharura mkewe kashikwa na kifafa cha mimba yuko hapo Masana, anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa haraka kuokoa maisha ya mama na mtoto!, zinahitajika shilingi laki mbili za dhamana tuu ili oparation ianze, anahitaji kuazima ili kuokoa tuu maisha ya wife wake na mchana by saa 8 atanirudishia!.
Kwa jinsi alivyo smart, anatumia piki piki ya hero mpya na kuongea kwa huruma, very convincing, nikamuamini, nikamwambia asubiri, na mimi nikarudi ndani kama zuzu, nikamuita wife aniletee laki mbili, zikaletwa, nikamkaribisha ndani, akasema shauri ya emergence ange prefer kusubiria tuu hapo hapo nje na sio mambo tena ya kuingia ndani kukaa!.
wakati nampelekea pesa, nikajiuliza hivi ni lini nilikwenda kituo cha polisi Mbezi kwa shida yoyote?, mimi na polisi zilikua enzi zile naendesha boda boda kama usafiri wangu, tangu nimeachana na boda boda na kutumia bajaj, nimekua sina isues na polisi!, lakini anyway, nikaamua ili kijiridhisha, kabla sijampa, huku nimeshika simu yangu ya voda, nikamuomba namba yake ya voda, nikajifanya nasave lakini nikatuma M-pesa ili kupata verification ya jina, likaja jina la Hassan Hassan, huku yeye alijitambulisha kama Afande Juma!. Nikasita kumpa kwanza zile pesa, nikamweleza kuwa fedha za kumpa tayari ninazo, naomba kitambulisho chake cha kuonyesha yeye ni polisi!, akajisearch, na kusema sorry amekisahau nyumbani katika haraka haraka ya kumkimbiza mgonjwa hospitali, nikamuuliza nitakupaje pesa bila kujua nampa nani?. Au anipe kitambulisho kingine chochote kuonyesha jina lake, akasema hana kitambulisho chochote, dharura za ugonjwa mtu huwezi hata kukumbuka kubeba kitambulisho!.
Nikampa option ya pili, kwa vile amesema yuko jirani, nikamshauri akalete kitambulisho chake cha polisi nimpe hiyo pesa!, jamaa aliondoka mnyonge na mpaka sasa imepita zaidi ya masaa hajarudi!.
Hawa jamaa kuna kitu wanatumia kukuingiza kingi haraka haraka nahisi ningekuwa na cash mfukoni, ningetapeliwa, kitendo cha kurudi tuu ndani, kutafuta pesa na kutoka tena nje, nikawa nimezinduka akili zakanirudia!. Yaani kwa jinsi pesa ilivyo ngumu, halafu mtu from nowhere humjui, hakujui, anakuja tuu kwako kubisha hodi getini, na kukuomba pesa kwa kutaja figure, kisha unaamua kumpa tuu just like that!, sii bure!.
Tuwe waangalifu sana na hawa matapeli na mbinu mpya za utapeli!.
Jumapili njema!.
Pasco

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!