Wednesday, 5 August 2015

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 WAWASILISHA MIRADI YAO YA KILIMO NA MAZINGIRA KWA WANAKIJIJI WA KISANGA WILAYANI KISARAWE PWANI‏


 Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwa katika Bwawa la Lamboni wakipata maelezo kutoka kwa wanakijiji hii ikiwa ni moja ya sehemu ya ziara yao jana .



 Wenyeji pamoja na  Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakielekea Mabondeni..Ilikuwa ni nafasi yao ya kufahamu maeneo mbalimbali Kijijini hapo...
 Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula wakioneshwa Madhari ya shule ya Msingi ya Kisanga na mmoja wa wanakijiji aliyesimama Mbele Kulia.
 Hapa washiriki wa Shindano la Mama Shijaa wa chakula 2o15 linalo andaliwa na Oxfam kupitia kampeni yao ya Grow , kipindi kinachoruka kila siku ITV kuanzia Saa Kumi na mbili  Jioni na Kurudiwa saa Tano na nusu asubuhi  wakiwa katika ofisi ya Kusindika zao la Mihogo
 Hapa washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 msimu wa nne wakiwa katika moja ya kisima ambacho maji yake yananukia Mafuta, maji haya yanatumika zaidi katika shughuli za Kufulia Nguo.
 Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona aliyesimama (Kulia) akizungumza na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Pamoja na wanakijiji katika Kijiji Cha Kisanga jana.
 Kundi la kwanza la Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Mazingira..
 Wanakijiji na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasikiliza jinsi Miradi inavyo wasilishwa.
 Kundi la pili la washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Kilimo Bora.

 Kundi la Tatu la washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Kilimo Bora cha Mboga Mboga na Hihogo.
********
Ni siku nyingine tena katika kijiji cha Kisanga, jua la saa nne asubuhi ni kali huku  mti huu mkubwa wa mkorosho uliopo eneo la makutano unatusitiri. Washiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula Shindano lililiondaliwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow, walikuwa wamesimama vikundi vikundi, bila shaka walikuwa wanahadithiana chakula walichowapikia wenyeji wao jana. 

Siku ya ilikuwa  inaanza kwa waandaaji wa shindano kutengeneza makundi matatu ya kina Mama Shujaa wa Chakula watano watano. 

Kwa muda watakaokaa hapa kijijini Kisanga, kila kundi linatakiwa kutengeneza mradi wa maendeleo endelevu kwa manufaa ya kijiji cha Kisanga. Ili kufahamu fursa na changamoto zilizopo, uongozi wa kijiji unawatembeza sehemu nne. 

Upatikanaji wa maji ya uhakika kijijini hapa ni changamoto. Kina Mama Shujaa wa Chakula wanaletwa sehemu hii yenye bwawa, wenyeji wanaiita lamboni. Inasadikika kuwa zamani kulikuwa na kisima, ila kwa sasa kimefunikwa na wingi wa maji. Pia kuna viumbe wakali kama vile chatu. 

Elimu ya msingi katika kijijini Napo inatolewa katika shule ya msingi Kisanga. Wakina Mama Shujaa wa Chakula wanaoneshwa mandhari ya shule na mwenyeji. 

Wakazi wa kijiji cha Kisanga wanapata maji ya kunywa na kupikia katika visima vilivyopo eneo hili linaloitwa Mfuru. Kufuatia msimu wa mvua ulioisha, visima vyote vinne vina maji ya kutosha, japo kisima kimoja maji yake hayatumiwi kwa kunywa kwani yana harufu inayosadikika kuwa ni ya mafuta. Hata hivyo, wakati wa kiangazi kina mama (wenyeji) wanalazimika kuamka saa tisa alfajiri kutokana na uhaba wa maji, na kibaya zaidi usalama wao wakiwa njiani ni wa mashaka kwani hawapewi msaada na waume zao (kwa walioolewa). 

Ziara ya kutembelea kijiji inafika kwenye hospitali/kituo cha afya cha Kisanga. Kina Mama shujaa wa chakula wanashangaa kuambiwa bei kubwa ya matibabu katika kituo hicho, ambacho kwa siku ya leo kimefungwa. 

Zao kuu la Kisanga ni mihogo. Ziara ya kina Mama Shujaa wa Chakula inaishia katika kituo cha kusindika mihogo. Hapa kunasagwa unga wa mihogo, pia tambi na keki za unga wa mihogo zinatengenezwa hapa. 

Naam, muda wa makundi kuwasilisha mapendekezo ya mradi wa maendeleo endelevu waliopanga mbele ya wanakijiji wa Kisanga unawadia.

KUNDI LA KWANZA 

Kutoa elimu juu ya mazingira, Kuchimba mashimo ya taka. Wafanyabiashara wanawake walio barabarani wafunike chakula ili vumbi lisiingie.Wana Kisanga wote watahitajika kufanya usafi jumamosi.  Kuanzisha shamba darasa na kutoa elimu.

KUNDI LA PILI
Biashara cha mboga na matunda kwenye bonde (karibu na bwawa) kwa kutumia mbolea asili na maji yaliyopo. Kutoa elimu kwa kupitia shamba darasa jinsi ya kutumia rasilimali za kijiji kwa ajili ya maendeleo ya kijiji

KUNDI LA TATU
Mradi wa kilimo bora. Kilimo cha mbogamboga na kilimo cha mihogo na mahindi kwenye muinuko wa bonde. Wananchi kupewa elimu ya kilimo bora, kutumia wataalamu waliopo

Siku inaisha kwa waandaaji kupanga makundi matatu mapya ambayo watapewa kazi ambayo lazima iishe kesho hiyohiyo.

ILI KUMPIGIA KURA MSHIRIKI  BOFYA HAPA

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!