Baadhi ya washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwa katika Sherehe ya kukaribishwa jana katika Kijiji cha Makumbusho.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster wa kwanza kulia akibadilishana mawazo na baadhi ya akina mama ambao watakuwa wenyeji wa wageni washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015
Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa ufupi juu ya Mchakato mzima wa Shindano la Mama shujaa wa chakula ambalo linalenga kuwawezesha wakina mama kutambulika katika kilimo na kueleza Matakwa yao juu ya kilimo endelevu.

Burudani ikiwa inaendelea wakati wa Sherehe za Kuwakaribisha na kuwatambulisha Rasmi Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo limeanza rasmi katika kijiji cha Kasanga wilayani Kisalawe
Bw. Godia Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Kasanga akiwakaribisha Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Shindano Linaloendeshwa na Oxfam Tanzania kupitia Kampeni ya Grow Kijijini kwake.
Bw. Godia Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Kasanga akiwakaribisha Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Shindano Linaloendeshwa na Oxfam Tanzania kupitia Kampeni ya Grow Kijijini kwake.
Bi. Mwanaidi Hamza ambaye anatoka katika Programu ya Big Result now
akitoa ushuhuda jinsi gani alivyofanikiwa kulingana na Proramu hiyo na
sasa anamaisha mazuri, na kuwasihi wakina mama wasikate tamaa katika
kilimo.
Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw.
Jackson Samwel akiwapongeza Shirika la Oxfam kupitia kampeni yake ya
Grow kuanzisha shindano la Mama shujaa wa Chakula , kwa kutambua umuhimu
wa ardhi katika kuzalisha chakula, ameshauri akinamama wabadilishane
uzoefu pindi watakapokuwa kambini ili kuja na mbinu mpya za kilimo,
ufugaji na uvuvi.
Stephen Mfuko aka Zero akitaja namba za washiriki na Jinsi ambavyo wanaweza Pigiwa Kura ambapo Programu mzima itaoneshwa katika Runinga ya ITV kila Siku kuanzia Tarehe 2.08.2015-21.08.2015 kuanzia saa 12 Jioni.

Baadhi ya washiriki wengine wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakifurahia jambo katika Sherehe hizo.
Baadhi ya Wageni waalikwa Pamoja na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula linaloandaliwa na Oxfam kupitia Programu ya Grow wakiwa katika sherehe za kuwakaribisha na kuwatambulisha washiriki hao
Mmoja wa Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula aliye vaa Tshirt nyeupe(wa pili kulia) ambalo litaanza kuruka kupitia Runinga ya ITV Kila siku kuanzia 2.08.2015 -21.08.2015 saa 12 Jioni akicheza ngoma ya kwao wakati wakitambulishwa
Mkurugenzi
Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiwashukuru wadau mbalimbali ambao
wamefanikisha mchakato mzima wa kuendesha shindano la Mama Shujaa wa
Chakula, Pia Kipekee Amewashukuru wafanyakazi wa Oxfam akiwepo Eluka
Kibona na Suhaila Thawer kwa kuwa Mstari wa mbele kufanikisha Shindano
hili na Mwisho kuwatakia kila Laheri washiriki wote wanaokwenda katika
kushindana kumpata Mama Shujaa wa Chakula.
Wakina Mama ambao ni Washiriki wa shindano la Kumsaka Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwa wanasema ile 'Slogan' yao ya "Mimi Mama, Najiamini, ewe mama Jitume Pamoja Tunaweza"
Baadhi ya akina Mama ambao ndio watakuwa wenyeji wa washiriki wa shindano la Kumsaka Mama Shujaa wa chakula 2015 ambalo linaandaliwa na Oxfam chini ya Kampeni ya Grow.
No comments:
Post a Comment