Thursday, 27 August 2015

VYAKULA VINAVYOCHANGIA KUZALIZA MAZIWA YA MAMA KWA WINGI

Kwa Mama anaenyonyesha ni kawaida kupungukiwa na maziwa pindi anyonyeshapo,kwa wazazi wengi wanapotoka kujifungua maziwa hutoka kidogo sana, wengine hukata tamaa ya kunyonyesha na  kuanzishia watoto maziwa ya kopo.


 

Hapana hilo ni kosa kinachotakiwa ni kumwachia mtoto anyonye hata kama hayatoki  iyo inafanya kustimulate(kuchochea) yatoke kwa urahisi .Mama anahitaji mda wa kupumzisha mwili na kula mlo wenye virutubisho,uzalishwaji wa maziwa hauwezi kwenda vizuri kama mwili una stress au haujapumzishwa vizuri.



Lishe bora itamfanya mama azalishe maziwa mengi anatakiwa kula milo 3-4 kwa siku,mama anaenyonyesha anatakiwa kula bila kuwazia atanenepa,cha muhimu kwanza ni mtoto apate maziwa ,mwili utakuja pungua wenyewe taratibu mtoto akishafika miezi 6 na kuendelea pale atakapo kula vyakula vingine (solid food).



Mlo wa mama anaenyonyesha unatakiwa kuwa

  • Maji yanahitajika kwa wingi ili maziwa yazalishwe ,kunywa maji glass 7-8 kwa siku

  • Matunda,mama ule matunda aina 2-3 tofauti kila siku

  • Mboga za majani kwa wingi,kila siku ulapo lunch au dinner

  • Mbegu-mama anatakiwa kula mboga jamii ya maharagwe,njegere,choroko,dengu n.k

  • Nyama,samaki na kuku

  • Viazi,maboga,mihogo na magimbi

  • Dairy products kama maziwa,cheese au mtindi

  • Ngano kama chapati,mkate,maandazi n.k

  • Mchele,mahindi,oats n.k

  • Tafuna mahindi,karanga na korosho

image

Njia ya kumwongezea mama maziwa

Uzalishaji wa maziwa wa mama unaweza kuongezwa kwa kutumia


  • Uji wa pilipili manga-utapika ujimwepesi  changanya na pilipili manga ,kunywa mara 2 kwa siku asubuhi na jioni.

  • Mbegu za maboga-unaweza zitafuta au kuchanganya kwenye uji au chai.

  • Juice ya karoti changanya na tangawizi kunywa mara 2 kwa siku

  • Tende-tafuna vipande vya tende 3 -4 kwa siku au toa mbegu ndani ya tende na saga kwenye blenda changanya na maziwa fresh kunywa mara 2 kwa siku.

  • Supu ya samaki au nyama iliochanganywa na mboga mboga kunywa mara 1 kwa siku.


image

Maji ya kunywa ni muhimu zaidi kunywa kwa wingi .

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!