Polisi mkoani hapa wamefanikiwa kuwauwa majambazi wawili baada ya kutupiana nao risasi kwa zaidi ya dakika 10.
Majambazi hao ambao walikuwa wanne wanadaiwa kutaka kufanya uhalifu kwenye Kisiwa cha Chembaya kilichopo katika Ziwa Victoria juzi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mwanza, Charles Mkumbo majambazi hao walikuwa wanatumia usafiri wa pikipiki na kwamba walianza kutupiana risasi na polisi baada ya kubaini kuwa wanafuatiliwa na askari waliopata taarifa dhidi yao.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda amesema polisi walipata taarifa saa 8:00 mchana juzi kutoka kwa raia wema kwamba kuna kikundi cha majambazi kinajiaanda kufanya uhalifu Ziwa Victoria.
“Baada ya Polisi kupata taarifa hizo walijipanga na kuweka mtego kwenye eneo la mwalo wa Kisaka uliyopo katika Kata ya Ilemela,” Kamanda Mkumbo amesema na kuongeza:
Kwa mujibu wa jeshi hilo, silaha moja aina ya Shotgun iliyofutwa namba na kukatwa kitako na mtutu wake zimepatikana baada ya majambazi hao kupekuliwa walikutwa na riasi tano.
Kamanda Mkumbo amesema miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Bugando, jijini Mwanza.
MWANANCHI.
MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment