Mtu mmoja amefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu na wengine watatu wamelazwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro ambao kati yao watatu ni familiya moja na mmoja ni familya nyingine.
ITV imefika hospitalini hapo nakukuta madaktari wakiwa katika juhudi za kuokoa maisha ya wagonjwa hao ambapo mganga mfawidhi wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Dr Ritha Lyamuya amesema kuingia kwa ugonjwa wa kipindupindu mkoani hapa nakuwataka wananchi kuchukua tahadhari.
Nao baadhi ya wananchi wametoa maoni yao kuhusu ugonjwa huu hatari na wameiomba serikali kutoa elimu kwa wananchi wake pamoja na kutafuta vitendea kazi hasa kwa watu wanaofanya kazi za kuzoa taka na kuhakikisha mji unasafishwa na kuwa safi ili kujikinga na ugonjwa huo wa hatari.
No comments:
Post a Comment