Watoto watano wa Tanzania wenye ulemavu wa ngozi waliokuwa wamekatwa viungo vya miili yao wamewekewa mikono na miguu ya bandia katika hospitali iliyopo nchini Marekani.
Watoto hawa ni miongoni mwa mamia ya watu wanye ulemavu wa ngozi nchini humo ambao wamekuwa wakiwindwa na watu wanaotaka viungo vya miili yao kwa shughuli za kishirikina
Watoto hao, mmoja wa kike na wanne wa kiume kutoka mikoa ya Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi mwa Tanzania, wamekuwa wakipokea matibabu hayo katika hospitali ya watoto Philadelphia Shriners Hospital iliyopo jijini New York.
Wakiwa na umri kati ya miaka 6 hadi 18, wanne wa watoto hawa walipatwa na majeraha makubwa ya kukatwa mikono na miguu yao, huku mmoja wao akiwa amekatwa taya na meno.
Tayari watoto wanne wamekwisha wekewa mikono na miguu ya bandia, wakati yule aliyekatwa taya akitarajiwa matibabu yake kuchukua muda mrefu zaidi
Shirika la msaada la Kimarekani Global Medical Relief Fund linafadhili matibabu ya watoto hawa.
Ofisa kutoka shirika la Under the Same Sun Martin Haule anasema watoto wanaendelea vizuri na kwamba ni wenye furaha
Ameiambia BBC kwamba wanatarajiwa kurudi nyumbani Tanzania mnamo mwezi Septemba
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ulemavu wa ngozi unaathiri takribani mtu mmoja katika kila watu 15,000 nchini Tanzania.
Watu hawa wanawindwa kwa ajili ya viungo vyao, ambavyo vinatakiwa katika biashara haramu kwa matumizi ya shughuri za kishirikina
BBC.
No comments:
Post a Comment