Tuesday, 18 August 2015

MSAMA KUUOMBEA UCHAGUZI MKUU

msama
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Msama Promotions imeandaa Tamasha kubwa la kihistoria ambalo halikuwahi kufanyika tangu kupatikana uhuru wa nchi hii tangu mwaka 1961 la kuiombea Tanzania unaoelekea katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Alex Msama Tamasha hilo ambalo linatarajia litafanyika Oktoba 4 jijini Dar es Salaam.
Msama alisema tamasha hilo linatarajia kushirikisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili wa ndani na nje ya nchi ambao wanatamba katika tasnia ya muziki huo.
“Watanzania wajiandae kuiombea amani Tanzania kupitia muziki wa Injili hasa waimbaji mbalimbali wa kutoka nje ya Tanzania watashiriki katika tukio hilo muhimu ambalo bado tuko katika mchakato wa mahali tutakapofanyia,” alisema Msama na kuongeza.
“Tamasha hilo kubwa kimaudhui linakaribia Tamasha kubwa la Kusifu na Kuabudu la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka,” alisema Msama.
Aidha Msama alisema baada ya tamasha hilo kufanyika jijini Dar es Salaam, watahamishia maombi hayo katika majiji mengine manne lengo likiwa ni kuombea uchaguzi Mkuu.   
Alitaja nchi watakazotoka waimbaji watakaosindikiza  maombi hayo ni pamoja na Afrika Kusini, Rwanda, Kenya, Uganda, Zambia, Burundi na  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!