NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM.
Mkutano wa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, umeahirishwa hadi hapo utakapotangzwa tena.
Kabla ya kuanza kwa mkutano huo, Lipumba inadaiwa alikuwa na kikao na Wazee wa chama hicho, huku ikidaiwa kuwa anataka kujitoa katika chama hicho.
Hata hivyo mkutano huo wa Lipumba umeibua mijadala miongoni mwa wadau wa siasa na wanachama wa chama hicho waliofurika katika Makao Makuu wa chama hicho, yaliyopo Buguruni, Dar es Salaam.
Inaelezwa kuwa Lipumba alikuwa na mazungumzo na Wazee wa chama hicho, hivyo angezungumza na waandishi baada ya hapo, lakini mambo yakawa tofauti hadi ilipotangazwakuwa atazungumza na waandishi wa habari hapo itakapotangazwa tena.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, amekanusha taarifa hizo jana katika Mkutano wa Chadema uliomtangaza Edward Lowassa kuwa mgombea rasmi wa Urais kupitia vyama vinavounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
No comments:
Post a Comment