Wednesday, 5 August 2015

MICHEZO:DIRISHA LA USAJIRI KUFUNGWA AGOSTI 6


DIRISHA la Usajili kwa klabu za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili, linatarajiwa kufungwa Agosti 6 mwaka huu.
NA MOHAMED MHARIZO .


Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Baraka Kizuguto, amesema kuwa shirikisho hilo linavikumbusha vilabu vyote kufanya usajili wa wachezaji wao mapema kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo, ili kuondokana na usumbufu wa kufanya usajili dakika za mwisho.

Pindi dirisha hilo litakapofungwa Agosti 6, hakuna klabu au timu yoyote itakayofanya tena usajili wake, hivyo ni vyema vilabu vitahakikisha vinamaliza mausala ya usajili mapema kabla ya siku ya mwisho.
Mchuano mkali katika masuala ya usajili nchini Tanzania unahisisha vilabu vitatu vya Simba, Yanga na Azam, ambazo ndizo zenye nguvu.
Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania, wanatarajia kuvaana na Azam FC katika mechi ya Ngao ya Jamii, itakaoyochezwa Agosti 22 mwaka huu ambapo ligi imepangwa kuanza Septemba 12 mwaka huu. 

Caption:
Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!