Siku moja Chura alikuwa ameketi pembezoni mwa mfereji akipunga upepo, Ng’e alimjia na kusema:” samahani bwana Chura, natakakuvuka mfereji huu, lakini siwezi kuogelea, Je? Uko radhi kunibeba na kunivusha?”
Chura akajibu: lakini wewe ni Ng’e na mimi ni Chura na kwakawaida Ng’e humdhuru Chura.
Nge akasema: kwanini nikudhuru ili hali nataka univushe mferji huu?
Chura akasema : vizuri! Sasa panda mgongoni kwangu nikuvushe?
Walipokuwa katika ya mfereji wakivuka, Ng’e akamdhuru chura.
Chura katika hali ya kutapatapa ikimtoka roho alisema: kwanini umefanya hivi? ona sasa sote tunazama!!.
Ng’e akamjibu: mimi ni Ng’e na wewe ni Chura, na kwa kawaida Ng’e humdhuru Chura!!.
Chura akakata roho na wote wakazama.
Katika maisha yetu pia, kunawatu wanatabia kama za Ng’e : wapo tayari kuweka maisha yao hatarini, au hata kupoteza maisha yao ili mradi wakuharibie mambo yako.
1 comment:
Nickysony Michael07:50
1
nice-hadithi
Post a Comment