Monday, 31 August 2015

KOMAMANGA HUZUIA KUSAMBAA KWA KANSA YA MATITI


Uchunguzi mpya umeonyesha kwamba, katika tunda la komamanga kuna kemikali zinazozuia kansa ya matiti kusambaa mwilini. Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarada la Utafiti la Kuzuia Kansa umeonyesha kwamba, kemikali ziitwazo ellegitannins zinazopatikana kwa wingi kwenye komamanga, zinaweza kuzuia kimeng'enyo (enzyme) aina ya aromatase, suala ambalo huzuia kukua kwa homoni ya estrogen inayopatikana katika kansa ya matiti.



 Shiuan Chen aliyeongoza uchunguzi huo amesema kwamba, kemikali hizo hupunguza uzalishwaji wa estrogen, na kusaidia kuzuia seli za kansa ya matiti kuzaliana mwilini pamoja na tezi la ugonjwa huo kukua.

Aromatase ni kimeng'enyo ambacho hugeuza homoni ya androgen kuwa estrogen, na kushambuliwa kimeng'enyo hicho ndio lengo kuu la dawa za kupambana na kansa za matiti zinazosababishwa na homoni ya etrogen.
Huko nyuma pia uchunguzi ulionyesha kwamba tunda la komamanga lina faida kubwa kiafya hasa kwa kuwa na antioxidant nyingi na vitamini mbalimbali, ambazo hulifanya tunda hilo liweze kusaidia katika mapambano dhidi ya magonjwa ya saratani, matatizo ya moyo na hata ugonjwa wa kusahau uzeeni au Alzheimer. Antioxidant huzuia radikali huru ambazo ni hatari sana kwa miili yetu. Uwezo huo huufanya mwili uweze kukabiliana na magonjwa mbalimbali hata ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe.  Hivyo ndugu msikilizaji kutokana na faida nyingi za tunda hili, kama huwezi kulipata sokoni, basi unaweza kutumia juisi yake na daima kuitunza afya yako. Faida nyinginezo za juisi ya komamanga ni,
Huzuia maendeleo ya saratani ya mapafu.Hupambana na saratani ya matitiHupunguza ukuaji wa saratani ya kibofuInaweza kuzuia na kupunguza kasi ya ugonjwa wa AlzheimerInapunguza  mafuta mwiliniHushusha shinikizo la damuHulinda meno
Inasemekana kwamba ukinywa juisi ya komamanga (pomegranate) nusu lita kila siku kwa muda wa mwezi mmoja, inasaidia kupunguza mafuta tumboni kwa wale wenye vitambi.      

Utafiti mwingine unatujuza kwamba, kutembea kunaweza kupunguza hatari ya kupata kansa ya matiti.  Utafiti huo mpya uliofanywa na timu ya Jamii ya Saratani ya Marekani umeonesha kuwa, kufanya mazoezi kama vile kutembea kwa miguu, kunaweza kupunguza hatari ya kupata kansa ya matiti kwa wanawake ambao hawapati tena hedhi. Utafiti huo umeonesha kuwa, kutembea kwa saa moja kila siku hupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya kupata ugonjwa huo. Timu hiyo ya watafiti iliwachunguza wanawake zaidi ya 73,000 walio na umri wa kuanzia miaka 50 hadi 74 na matokeo yameonesha kuwa, wanawake waliotembea kwa masaa yasiyopungua 7 kwa wiki walipunguza hatari ya kupata kansa ya matiti kwa asilimia 14 ikilinganishwa na wale waliotembea kwa masaa matatu au chini ya hapo.
Dakta Baroness Delyth Morgan Mkurugenzi Mkuu wa Kampeni ya Kupambana na Saratani ya Matiti amesema kuwa, kwa mara nyingine utafiti huo umesisitiza jinsi mfumo wa maisha ya mtu unavyoweza kuathiri hatari ya kupata ugonjwa wa kensa ya matiti.



Hali kadhalika wataalamu wanatuambia kuwa mammography inaweza kuokoa maisha ya wanawake wengi. Japokuwa kumekuwepo na mjadala mkubwa kuhusu uwezo wa kutambua ugonjwa wa kipimo kinachotumiwa kugundua kansa ya matiti, lakini utafiti umethibitsiha kwamba kipimo hicho kina faida kubwa. Uchunguzi huo umeonesha kuwa, kipimo cha mammography kina faida kubwa zaidi kuliko hasara zake, na kwamba kutumiwa kwake kunaokoa zaidi maisha ya wanawake yanayoweza kupotea kutokana na kansa ya matiti.  Ijapokuwa mammography ina uwezo wa kuonyesha uvimbe (tumors), lakini pia kipimo hicho kinaweza kuonyesha uvimbe ambao hauna madhara na kuwafanya baadhi ya wanawake wapate wasiwasi na kufanyiwa operesheni bila kuwa na tatizo. Uchunguzi wa huko nyuma ulishauri kuwa, umri wa kufanyiwa kipimo cha mammography ili kujua kama mtu ana saratani ya matiti au la usogezwe kutoka miaka 40 hadi 50 ili kupunguza uwezekano wa wanawake kufanyiwa kipimo hicho mara nyingi maishani. Vilevile imesisitiza kwamba, kwa kila wanawake 6 ambao hufanyiwa kipimo hicho bila ya kuwa na ulazima, kuna maisha ya mwanamke mmoja yanayonusuriwa kwa kufanyiwa mammography.
Kwa hivyo wataalamu wamewashauri wanawake wasizembee na kuwahimiza wafanyiwe kipimo hicho, kwani faida zake ni kubwa zaidi kuliko hasara. Si vibaya kujua kuwa, nchini Uingereza pekee zaidi ya wanawake 45,000 hugunduliwa kuwa na saratani ya matiti kila mwaka, na zaidi ya wanawake 12,000 hufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.



FAIDA ZA KOMAMANGA:
1. Kuongeza na kusafisha damu.
2. Husafisha ngozi na kuifanya iwe nyororo.
3. Husafisha figo.
4. Hupunguza uzito kwa wanene pia hupunguza mafuta mwilini.
5. Hukabiliana na saratani na kuzuia kasi ya saratani kusambaa.
6. Hukabiliana na matatizo ya moyo.
7. Huongeza nguvu za kiume.
8. Husaidia katika mpangilio wa siku za wanawake.
9. Huongeza nguvu ya kumbukumbu.
10. Hutibu magonjwa ya tumbo.
11. Hulinda meno.

VIRUTUBISHO NA VITAMINI ZA TUNDA HILI:
VIPIMO HINI NI KWA KILA GRAMU MIA 100 g (3.5 oz)
Energy346 kJ (83 kcal)
Carbohydrates18.7 g
Sugars13.67 g
Dietary fiber4 g
Fat1.17 g
Protein1.67 g
Thiamine (vit. B1)0.067 mg (6%)
Riboflavin (vit. B2)0.053 mg (4%)
Niacin (vit. B3)0.293 mg (2%)
Pantothenic acid (B5)0.377 mg (8%)
Vitamin B60.075 mg (6%)
Folate (vit. B9)38 μg (10%)
Choline7.6 mg (2%)
Vitamin C10.2 mg (12%)
Vitamin E0.6 mg (4%)
Vitamin K16.4 μg (16%)
Calcium10 mg (1%)
Iron0.3 mg (2%)
Magnesium12 mg (3%)
Manganese0.119 mg (6%)
Phosphorus36 mg (5%)
Potassium236 mg (5%)
Sodium3 mg (0%)
Zinc0.35 mg (4%)


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!