Watu wanne wafariki dunia hapohapo nawengine kujeruhiwa mara baada ya basi la sabuni expres linalofanya safarizake kutoka wilayani karagwe kwenda mwanza jijini kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya landcrusezer iliyokuwa ikiwasafirisha mapadri kutoka bukoba kuelekea karagwe katika eneo la bugorola wilayan misenyi.
Ajali hiyo imetokea majira sambili asubuhi katika eneo la Bugorola wilayani Misenyi ambapo baadhi mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo imetokea wakati Dereva wa gari ndogo aina ya landcruser alipokuwa akijaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake na kisha kukutana uso kwa uso na basi la Sabuni Express lililokuwa na biria wapatao arobani na tano na kusabisha vifo vya watu wanne ambao ni mapadri wawili,Sister mmoja na mseminalisti mmoja wote walikuwa wakisafiri na gari hiyo kuelekea karagwe.
Wakizungumza na ITV baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri na basi hilo wamsema dereva wa basi alikuwa katika mwendo wa kawaida kutokana ukungu ulikuwa kuwa umetenda barabarani.
Kwa upande wake katibu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa kagera Kiiza Kilwanila amesema wamepokea maiti nne pamoja na majeruhi kadhaa ambao sasa halizao zinaendelea vizuri.
ITV imefika katika kituo chapolisi mkoani Kagera kwaajili kuthibitisha tukio hilo kwa kamanda wajeshi ambapo sikuweza kumkuta na kujaribu kumtafuta kwa njia ya simu hakuweza kupatikana.
CHANZO ITV.
No comments:
Post a Comment