Tuesday, 28 July 2015

TAMBI ZA MAYAI!

TAMBI ZA MAYAI

Licha ya utamu wa chakula hiki,kitu kingine ninachopenda  ni muonekano wake hasa ambavyo mayai hutengeneza kama matone madogo madogo na kushikana na tambi.

Mahitaji
  • Tambi  ½ paketi
  • Vitunguu maji 2 vikubwa

  • Karoti 1
  • Hoho 1
  • Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
  • Carry powder kijiko 1 cha chai
  • Njegere zilizochemshwa ½ kikombe
  • Mafuta kwa kiasi upendacho
  • Mayai 2
  • Chumvi kwa ladha upendayo
Njia
1.Chemsha maji yamoto yanayotokota,ongeza chumvi na mafuta kidogo,weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive.Chuja maji yote ili kupata tambi kavu
2.Katika bakuli piga mayai kisha weka  pembeni
3.Katika kikaango,weka mafuta,vitunguu maji ,vitunguu swaumu,hoho, karoti  na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo  kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva.
4.Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya .
5.Ongeza mayai kwenye  tambi  kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi  ziwe kavu.Tayari kwa kula
  • Katika hatua hii ongeza moto uwe wa wastani,moto ukiwa mdogo mayai yatafanya tambi zishikane na kufanya mabonge.
Unaweza kula tambi hizi na mboga yoyote upendayo au laa ukala zikiwa kavu na kufuraia ladha yake zaidi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!