Ikiwa ni saa chache baada ya Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatterkutangaza kuwa atajiuzulu wadhifa huo kuna habari nyingine zinamuhusu Rais huyo.
Rais huyo ambaye alipewa madaraka ya kuongoza Shirikisho hilo siku chache zilizopita ikiwa ni awamu ya tano, kuna taarifa kuwa Sepp Blatter anafanyiwa uchunguzi na maafisa wa marekani ili kuthibitisha tuhuma za rushwa zinazomkabili kwa sasa yeye na watendaji wake.
Waendesha mashtaka Marekani wanaofuatilia tuhuma za rushwa walikamata maafisa saba wa FIFA nchini Switzerland kati ya watu 14 wanaotuhumiwa kwenye kashfa hiyo.
Hata hivyo Blatter alisema anatumia mamlaka aliyopewa hata kama hayakubaliwi na kila mtu duniani.
Fifa inahitaji mabadiliko makubwa kwa sasa ili kukemea rushwa.
Hata hivyo Blatter amesema ataendeleaa kukaa madarakani hadi utakapoitishwa mkutano wa kumpata Rais mwingine ambao huenda ukafanyika Desemba mwaka huu au March mwakani.
Katika taarifa iliyoripotiwa kutoka kwa maafisa wa Marekani wiki iliyopita kuhusu rushwa katika shirikisho hilo la soka ulimwenguni, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Loretta Lynch haikumshutumu Blatter moja kwa moja .
No comments:
Post a Comment