Wednesday, 10 June 2015

MAFUNZO YA KUANDAA CHAKULA CHA WATOTO TOKA KATIKA RATIBA



KIFUNGUA KINYWA ( BREAKFAST)


CHAPATI MAJI NA JUISI YA CHUNGWA

250 gram Unga wa ngano
1 yai
100 gram maziwa ya maji
20 gram mafuta ya mahindi
10 gram baking powder

Jinsi ya kuandaa chapati maji changanya vitu vyote katika bakulikisha piga na mchapo mpaka upate mchanganyiko safi na laini kabisa kama mchanganyiko bado mzito ongeza maji kiasi.

Jinsi ya kuandaa juisi ya chungwa. Menya chunga safi kabisa ili kundoa uchungu wa gesi iliyopo katika maganda. kisha tumia chombo maalumu cha kukamulia juice kamua kisha hifadhi katika friji bila kuweka sukari ili ikae kwa muda isiharibike kumbuka kuweka sukari wakati wa kunywa.

UJI ULEZI NA MTINDI

200 gram unga wa ulezi
100 gram maziwa ya maji
350 gram maji
100 gram mtindi usio na ladha ya matunda

Changanya unga wa ulezi na maziwa katika bakuli kisha chukua sufuria weka maji hiyo gram 300 chemsha yakisha chemka weka mchanganyiko wa maziwa na unga wa ulezi koroga mpaka uchemke na kuchanganyika safi kabisa ili uji wako usishike chini na kuungua. Acha uchemke vizuri kisha onja ukipata ladha ya kuiva kwa nafaka utakua tayari.
Toa jikoni weka kaitka bakuli atakalo tumia mtoto kisha changaya mtindi usio na ladha yamatunda pamoja na sukati tayari kwa mtoto kunywa.

 CHAKULA CHA MCHANA


 GLASI YA MAZIWA NA MKATE WA NYAMA ZA KUSINDIKA

Mpatie mtoto 200 gram ya maziwa swa na glasi moja ya uvugu vugu au ya baridi lakini kumbuka yawe yamechemshwa vizuri na yakapoa kwajili ya usalama.

Kisha chukua vipande viwili vya mkate paka siagi au mayonaisi. Kisha chukua beef salami na beef backon weka kati kati pamoja na slice ya nyanya na tango mbichi mpatie mtoto ale.

 KITAFUNWA CHA JIONI 


 SAHANI YA MCHANGANYIKO WA MBOGA MBICHI

chukua caroti, tango, pili pili hoho  nyekundu na ya kijani zote mbichi na zuchini ichemshe kidogo kisha weka mtindi wenye ladha ya matunda kwajili ya kulia hizo mboga.


Huu ndio muonekano wa sahani ya mchanganyiko wa mboga kama mtoto ni mdogo sana zisage kwenye mashine ya kusagia nyama kisha utapata mchanganyiko laini mpatie mtoto asieweza kutafuna hizo mboga mbichi.

 CHAKULA CHA USIKU


 SUPU YA UYOGA, KUKU MAZIWA wa MIHOGO NA NJEGERE


Mahitaji ya Supu ya uyoga

300gram Uyoga fresh au wa kopo
50 gram kitunguu maji
10 gram kitunguu swaumu
10 gram tangawizi
50 gram leeks
100 gram viazi ulaya
100 gram maziwa fresh
50 gram mafuta ya kupikia
300 gram maji

Kaanga katika mafuta ya kupikia vitunguu maji na vitunguu swaumu pamoja na tangawizi. kisah weka viazi ulaya, leeks na uyoga kaanga tena kiasi kisha weka maziwa na maji acha ichemke mpaka viazi viive kisha toa na saga kwenye blenda rudisha jikoni kama nzito san ongeza maziwa au maji kiasi kumbuka kuweka chumvi kkulingana na ladha.

Mahitaji ya kuku wa maziwa, muhogo na njegere

200 gram nyama ya kuku isiyo na mifupa
100 gram njegere
200 gram maziwa 
150 mihogo iliyochemshwa kwanza
300 gram maji


Hii ndio machine ya kusagia nyama utakayoitumia kwajili ya kusagia chakula mbali mbali.

Chemsha vyote kwa pamoja kuku na njegere mbichi pamoja na muhogo uliokwisha chemshwa kwanza mpaka ikaribie kukauka mchuzi  kisha toa chuja mchuzi weka pembeni.

Chukua mchanganyiko wa njegere, kuku na muhogo tumia machine ya kusagia nyama weka saga upate rojo zito kisha rudisha katika sufuri changanya na ule mchuzi uliochuja ongeza chumvi kulingana na ladha mpe mtoto ale chakula kikiwa cha moto.

Kama hauna mashine ya kusagia nyama tumia mwiko kuponda itakua safi kabisa kisha unachangaya na ule mchuzi uliochuja.

Kwa mtoto mkubwa usisage baada ya kuchemsha ikaiva oneza chumvi kisha mpakulie ale chakula chamoto atafurahia sana mchanganyiko wa ladha ya chakula hiki.


Uyoga wa kopo au fresh, Mihogo mibichi, pili pili hoho, tangawizi, Unga wa ngano, Mayai, Maziwa, Sukari, Chumvi, Njegere, Nyama ya kuku, Tango, Zucchini, Mtindi usio na ladha ya matunda, Mtindi wa ladha ya matunda, Baking powder, Viazi ulaya, Mafuta ya mahindi na leeks.

Vitu hivi vyote sio vingi na unaweza kuvitumia siku inayofuata maana menu yetu inauwiano safi kabisa vitu vingi vinatumika baribu kila siku na manunuzi yake sio ghali kabisa mpe mwanao raha kwa kula chakula safi na salama.


Special thanks to Chief Issa

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!