Monday, 15 June 2015

AJALI YA BASI YAUA 10 IRINGA


Basi la Another G kutoka Njombe kwenda Iringa limepata ajali usiku huu eneo la Kinyanambo Mjini Mafinga baada ya kugongwa na Lori inadaiwa watu 10 wamepoteza Maisha




WATU zaidi ya 10 wamepoteza maisha usiku huu katika ajali ya gari aina ya costa mali ya Another G inayofanya safari zake kati ya Njombe - Iringa baada ya kugongana na Lori.


Taarifa za awali ambazo mtandao z umezipata kutoka eneo la tukio zinadai kuwa ajali hiyo imetokea eneo la Kinyanambo nje kidogo na mji wa Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wakati gari hiyo ya Another G ikitokea Njombe kwenda Iringa

Mbali ya kuwa maiti ambazo zimetolewa na kufikishwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya wilaya ya Mufindi kuwa zimekwisha fika zaidi ya 10 ila inadai kuwa idadi ya miili inaweza kuongezeka zaidi kutokana na kazi ya uokoaji ikiendelea eneo la tukio.

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita ameuthibitishia mtandao huu wa matukiodaima kwa njia ya simu juu ya ajali hiyo na kueleza kuwa ni miongoni mwa ajali mbaya kutokea wilayani Mufindi .

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!