Sunday, 3 May 2015

WANAWAKE 2000 KUPEWA ELIMU YA MADINI

index

KAMPUNI ya Kibua Juma Nguku inatarajia kutoa elimu ya madini kwa
wanawake zaidi ya 2000 kutoka katika mikoa ya Dar es salaam pamoja na
Tanga ambapo kupitia mafunzo hayo yataweza kuwasaidia kuongeza uelewa
zaidi wa biashara hiyo ya madiniKutokana na elimu hiyo ambayo watapewa pia wataweza kuepukana naa
tabia ya udanganganyifu ambao wanaupata kwenye sekta hiyo ya madini na
hivyo wanawake wengi kuona kuwa kazi hiyo ya madini ni maalumu kwa
ajili ya wanaume pekee.




Akiongea na gazeti hili mapema jana wakati wa maonesho ya vito vya
thamani  yaliyokuwa yakiendelea Jijini hapa mkurugenzi mtendaji wa
kampuni hiyo Kibua Nguku alidai kuwa mpango huop utafanywa na kampuni
yake hivi karibuni ambapo wanufaikaji wakubwa ni wanawake
Alidai, mafunzo hayo yatalenga mambo muhimu kama vile kukata
mawe,kutengeneza vizuri,pamoja na kuyaongezea thamani ambapo kama
wataweza kuyajua hayo yote basi watachangia sana kuongeza uchumi.
“kazi ya madini sio kazi ambayo wameumbiwa wanaume pekee bali hata
wanawake wana uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi hiyo na kisha
wakajikomboe kiuchumi lakini ni muhimu sasa wakawa na elimu”aliongeza
Kibua
Mbali na kuwapa elimu hiyo aliwataka wanawake sasa kutafuta fursa za
madini zilizopo hukuwa wakiwa na elimu kwani kama watakuwa na elimu ya
kutosha juu ya aina za madini basi hawataweza danganyika na baadhi ya
watu ambao ni wadanganyifu kwenye sekta hiyo.
Wakati huo huo aliiomba Serikali kuangalia soko la madini na vito vya
thamani ambavyo kwa sasa yanapatikana kwa wingi sana hapa nchini ila
soko lake kubwa lipo nje ya nchi jambo ambalo ni hasara kubwa  sana.
Kibua alifafanua kuwa wizi wa madini unafanyika sana na wanaoufanya
wizi huo wanasababisha wadau wa madini hapa nchini kujikuta wakiwa
wanawafanyia kazi baaadhi ya watu ambao wapo nje ya nchi kitu ambacho
ni hasara na uchumi hauwezi kukua kwa namna hiyo.
“ili biashara hii ya madini iweze kutusaidia sisi watanzania ni lazima
tafiti zifanyike na kisha Serikali ishirikiane na sisi kuwadhibiti
hawa wezi ambao wakati mwingine wanachangaia kuharibu soko na biashara
hii”aliongeza hivyo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!