Saturday, 9 May 2015

CAMERON ACHAGULIWA TENA

LONDON, ENGLAND - MAY 08:  Prime Minister David Cameron leaves for Downing Street on May 8, 2015 in London, England. After the United Kingdom went to the polls in a closely fought General Election the Conservative party, led by David Cameron, are expected to be the winning party with support for both the Labour party and the Liberal Democrats falling away throughout the country.  (Photo by Dan Kitwood/Getty Images)
Raia wa Uingereza jana walikuwa na kazi moja ya kumchagua kiongozi mpya atakayewaongoza kwa muhula mwingine baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.


Chama cha Conservatives kilikua na upinzani mkali dhidi ya Labour lakini kura ya Raia hao imeangukia kwa Waziri mkuu wa nchi hiyo David Cameron kushinda kiti cha kuongoza Taifa hilo kubwa duniani kupitia chama chake cha Conservatives.
David Cameron amechaguliwa kwa awamu ya pili na ushindi huo umekuja baada ya kushinda viti 323 alivyohitajika kushinda.
Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza,Ed Miliband amewaambia wanaharakati wa chama hicho kwamba anajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho kufuatia matokeo yasiyo ya haki ya uchaguzi huo.
David Cameron anarejea madarakani bila idadi kubwa ya wabunge kwa kuwa Chama cha Conservative kitalazimika kuunda serikali ya muungano.
Miliband amempongeza Waziri mkuu David Cameron kwa kuchaguliwa kwa awamu ya pili na amesema kuwa anachukua jukumu la kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi huo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!