Thursday 2 April 2015

KIJANA ACHINJA FAMILIA NA KUWALA


KIJANA mmoja raia wa Hong Kong amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mauaji, kutawanya viungo vya nduguze, kuwanyunyizia chumvi na kuwapika.



Mtuhumiwa huyo ana umri wa miaka 31 na ametambulika kwa jina la Henry Chau.

Kijana huyo aliibua hisia za walio wengi katika kesi ya namna yake mnamo 2013 wakati kichwa cha mama yake mkubwa pamoja na baba yake vilipobainika kuhifadhiwa katika majokofu mawili tofauti.

Kesi hiyo iliendeshwa katika mahakama kuu ya nchini humo iliyopo mjini Hong Kong ambapo alielezea jinsi alivyokuwa akiwaua nduguze.

Chau hutekeleza mauaji hayo ambapo kwanza huua, pili hutawanya viungo vya maiti na kisha huwanyunyizia chumvi ili kuongeza ladha ya nyama katika miili hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Xinua, Chau alisema kuwa anafanya hayo yote kutokana  na matokeo ya mapenzi yake kwa nyama choma ya kitimoto.

Chau alisema kuwa nyama hiyo ya binadamu ikishaiva ama kuchomwa huwa anafunga nyama hiyo katika makasha ya chakula pamoja na ubwabwa.

Polisi walipofanya upekuzi katika nyumba yake walikuta baadhi ya viungo vya binadamu katika chombo cha kuhifadhia taka.

Akitoa hukumu dhidi ya kesi hiyo, jaji Michael Stuart-Moore alimuelezea Chau kama mbinafsi mwenye msongo wa mawazo kutokana na mafanikio mabaya ya maisha yake na asiye na huruma kwa wengine.

Chau, alihukumiwa adhabu mbili ikiwa ni pamoja na kifungo cha maisha jela na miaka tisa na miezi minne kwa makosa mawili tofauti kwa kuvunja sheria ya kuzika miili ya familia yake isivyo kawaida kosa ambalo alilikiri baadaye.

Hapo awali rafiki wa Chau alikuwa akihusishwa katika mauaji hayo ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita alikutwa hana hatia.

Taarifa za kupotea kwa wanafamilia wa Chau zilipoibuliwa, Chau alidanganya kuwa jamaa zake walikuwa wamesafiri lakini baadaye alijisahau na kumuandikia rafiki yake kupitia ujumbe mfupi wa simu kwamba aliwaua jamaa zake.

Chau mwenyewe hujiita mwendawazimu katika ujumbe aliokuwa akiwatumia watu wake wa karibu alisema katika ujumbe huo kuwa hawezi kumuonea huruma mtu yeyote kutokana na maumivu aliyopitia wakati wa makuzi yake utotoni mpaka anakuwa mtu mzima.

Chau anasema kuwa aliamua kuwadanganya polisi ili apate wasaa wa kuwaaga marafiki zake.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!