Mwanzilishi wa Label ya Death Row, Mario "Suge" Knight jana alianguka mahakamani baada ya jaji kumtaka atoe dola milioni 25 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 45 za Kitanzania kawa ajili ya dhamana kwenye kesi yake ya mauaji, kiwango ambacho wakili wake amesema ni kikubwa mno.
Wakili wa Suge, alisema mteja wake hawezi kumudu kulipa kiasi hicho cha fedha ambacho Suge aliishiwa nguvu na kuanguka dakika chache baada ya kusikia taarifa hizo akiwa mahakamani hapo.
Awali jaji huyo alidai kuwa ana wasiwasi Suge anaweza kutoroka kwa kuwa alishawahi kufanya hivyo siku za nyuma. Knight anashikiliwa kwa kosa la kuwagonga kwa gari watu wawili na kumuua mmoja baada ya kutokea malumbano.
No comments:
Post a Comment