“Sitaisahau hii siku maishani mwangu, kutokana na mawazo, hofu na kero niliyoipata kutoka kwa mume wangu, watoto na hata majirani zangu ambao baadhi walikuwa wakisema eti nimeua wasichana 20 baada ya kuwakeketa.
Ilikuwa alfajiri nilipoamka na kuanza kazi ya kuwakeketa wasichana hao 20 nilioletewa na wazazi wao. Nilipoanza kuifanya hiyo kazi huku nikiwa tayari nimeshawakeketa wasichana 12, walianza kuishiwa nguvu na baadhi yao walikuwa wakitokwa na damu nyingi tofauti na wasichana wengine ambao nilikuwa nikiwakeketa kabla yao.
Cha kusikitisha zaidi, nilipomaliza kuwakeketa wote 20, hali zao zilikuwa mbaya na baadhi walizimia, huku damu nyingi zikiendelea kuwatoka.
Niliogopa sana…sikujua la kufanya lakini namshukuru Mungu alinihurumia, mabinti wale baadaye walizinduka na kupata fahamu. Tangu siku hiyo, niliapa kuwa sitafanya tena kazi hiyo ya ukeketaji maana niliona sasa kuna hatari ya kuja kuua.”
Hiyo ni kauli ya ngariba mstaafu Mariana Ndama (66), mkazi wa Kijiji cha Ikungi mkoani Dodoma.
Kwa Mariana, tukio hilo alilichukulia kuwa si la kawaida na hata aliwaza kuwa huenda wenzake wamemchezea mchezo mchafu wa kuroga kwa nia ya kutomtakia heri katika kazi yake hiyo.
Anasema ajali hiyo ya ukeketaji ilikuwa ya kwanza kwake tangu alipoanza kazi hiyo mwaka 1965, katika Kijiji cha Puma mkoani Dodoma.
Hakumbuki idadi halisi ya wasichana aliowakeketa kwa sababu hakuwa anatunza kumbukumbu, bali anakadiria kuwa ni zaidi ya 1,000.
“Nilikuwa nakeketa wasichana kuanzia watano mpaka 30 kwa wakati mmoja, hawa waliletwa nyumbani kwangu au wakati mwingine niliwafuata katika vijiji vyao. Niliitwa kwenda kufanya shughuli hiyo,” anasema.
Mariana anasema kilichomsukuma kuwa ngariba mkeketaji ni kwanza, kupunguza gharama za kuwalipa mangariba, wakati huo ilikuwa Sh2 kwa kila msichana.
Pili, alivutiwa kufanya kazi hiyo baada ya kuona bibi yake akiifanya, akisema faida yake aliona inaweza kumletea sifa ya ujasiri na kujulikana pia.
“Nilianza kufanya majaribio kwa watoto wangu mwenyewe ili kunijengea ujasiri wa kutowaonea huruma wasichana wengine. Nilipoona nimefanikiwa kuwakeketa binti zangu wawili ambao sasa wana wajukuu… basi nikaona ninaweza na kazi yangu ikawa rahisi kuwakeketa wasichana kwa sababu nilishakomaa. Sikuwa na huruma hata kidogo nilipokuwa nikiifanya kazi hiyo,” anasema.
Kuanzia hapo, watu wakamwamini na kuanza kumpelekea mabinti zao ili awakekete, naye alifanya kazi hiyo kikamilifu kwa malipo ya fedha na mifugo.
Vifaa
Kuhusu vifaa alivyokuwa akivitumia, Mariana anasema alikuwa akitumia chuma kilichopondwa, jiwe na wembe.
Anabainisha kuwa alikuwa akitumia kifaa kimoja kuketea wasichana wote kwa wakati mmoja.
Unavyofanyika
Akizungumzia mila hiyo inavyotekelezwa, ngariba huyo anasema wanawake wanne au watano humshika kwa nguvu msichana na kumtanua miguu yake kisha ngariba hufanya kazi yake.
Anasimulia kuwa baadhi mangariba hukata kidogo, lakini wengine hunyofoa sehemu kubwa ya via vya uzazi vya msichana, bila ya kujali kama damu nyingi inabubujika.
“Unapokatwa unasikia maumivu makali, baadhi hutaja majina ya baba, mama na bibi zao kwa sauti ya uchungu na kuomboleza. Lakini kwa kuwa ni mila, unajikaza na kutulia ili kazi ifanyike haraka na kwa ufanisi.
Ukimaliza kumkeketa binti, watu husherehekea kwa kucheza hata usiku kucha, huku wakinywa pombe,” anasema.
Mariana anasema kuwa, ukeketaji unafanyika kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kuwaandaa wasichana kuingia daraja la utu uzima, ili kukwawezesha kupata waume wa kuwaoa mapema kulingana na mila na desturi za kabila lake la Wanyaturu.
Anasema siku aliyokata shauri ya kuacha kufanya kazi hiyo ni pale alipowakeketa wasichana 20 ambao walizimia na mume wake alimnyooshea kidole akamwambia; “umependa kukeketa angalia sasa utakwenda jela watoto hao wakiangamia.”
Anasimulia kuwa baada ya wasichana hao kuzinduka na kurudi makwao, alipunguza kasi ya ukeketaji na kufikia mwaka 1985, aliamua kuacha kabisa.
“Baada ya kusikia matangazo yanayosema mila hiyo ni kinyume cha sheria na watakaokamatwa watachukuliwa hatua za kisheria na kuadhibiwa nikaacha kazi ya kukeketa,” anasema.
Mariana anaeleza kuwa sasa ameamua kuwa mwelimishaji kuhusu madhara ya ukeketaji huku akiwataka mangariba wote kuacha mara moja kazi hiyo ili kuepusha hatari inayowakumba wasichana wanaofanyiwa mila hiyo potofu.
“Acheni kazi hii ni mbaya sana… inaua. Ni janga kama Ukimwi. Wasichana wakikeketwa, baadhi hutokwa damu nyingi. Wakifa, ngariba utakamatwa, utapelekwa mahakamani na kunyongwa,” Mariana anatahadharisha na kuongeza:
“Hapo kijijini Ikungi kuna shule ya msingi yenye wanafunzi mchanganyiko wakiwamo walemavu na vipofu, nimemwomba mwalimu mkuu aniruhusu niwe nakwenda kufundisha kuhusu mila na desturi za kabila letu kwa wanafunzi wa madarasa ya tano na sita. Ninajuta kuwa ngariba.”
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ikungi (jina linahifadhiwa) anasema alikeketwa akiwa na umri wa miaka sita.
“Nilipelekwa kwa nguvu na kukamatwa na watu wengi…. nilitoka damu nyingi …kitendo kile sikukipenda, hadi sasa nikikumbuka hupata uchungu na kujiuliza kwa nini nilifanyiwa.
Kwa kuwa sasa umri wangu umeongezeka, nikisikia huko kijijini kuna mpango wa msichana kukeketwa hutoa taarifa haraka kwa wanaharakati ili kuokoa maisha ya wenzangu,” anasema binti huyo katika ushuhuda wake alivyoguswa na tukio hilo.
Mwalimu Mohammed Saidi wa Shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko anasema, shule yao imeanzisha klabu za uelimishaji ambazo hutoa elimu kuhusu madhara ya ukeketaji kwa wasichana ili waweze kujitambua na kuchukia kukeketwa, pia kutoa taarifa polisi inapobainika kuwa kuna mazingira kama hayo.
“Hatua hii inachangia kupunguza kuenea kwa vitendo hivyo katika jamii yetu ambayo bado inakumbatia mila hiyo potofu. Naiomba jamii iondokane na mila hiyo inayoendeleza ukatili kwa wasichana,” anasema.
Polisi mkoani Singida inasema kutokana na taarifa za kiintelijensia, imebaini kuwa mangariba wanatumia njia za siri zaidi kuwakeketa watoto wakiwa wachanga kwa kuwafunga kamba au uzi sehemu za siri ili zikatike zenyewe taratibu. Njia hii hutumika zaidi katika Kijiji cha Mtinko.

No comments:
Post a Comment