Bill Gate.Ndugu zangu, hakuna anayeweza kuupinga ukweli kwamba, maisha ya sasa ni magumu, ugumu ambao kama mtu atabweteka na kushindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo upo uwezekano mkubwa wa kujikuta anaingia katika mfumo wa maisha yasiyokuwa na mbele wala nyuma na ugumu huo wa maisha kuwa mara mbili yake.
Lakini licha ya ukweli huo, bado nafasi zipo wazi kwa watu kuingia katika ulimwengu wa mafanikio. Hii itatokea tu kama mtu ataamua kupambana ipasavyo na kuhakikisha haingii katika kapu la umaskini ambalo limejaa wengi hata wasiostahili kuwemo ndani ya kapu hilo.
Wapo watu na afya zao, nguvu za kutosha pamoja na maarifa waliyopewa na Mungu lakini bado wameridhika kuishi maisha ya kifukara huku wakitegemea misaada kutoka kwa watu wengine ili kuweza kusogeza siku.
Hakika hii ni hatari sana na uhatari huo unakuja hasa pale unapomuona mtu ambaye ana kila sababu ya kuwa miongoni mwa watu wenye mafanikio lakini yeye anaona hawezi kuwa hivyo huku akiwa na dhana kwamba, yeye ni miongoni mwa wale waliopangiwa kuishi maisha ya kifukara hadi mwisho wa maisha yao.
VIA-BLOG YA WANANCHI
No comments:
Post a Comment