Friday 20 March 2015

DAR ES SALAAM YAONGOZA KUVUTIA WAWEKEZAJI

 Jiji la Dar es Salaam limetajwa kuwa la kwanza kati ya majiji 20 yenye fursa zaidi barani Afrika likiongoza katika kipengele cha kuvutia wawekezaji na kipengele kidogo cha ukuaji wa pato la taifa (GDP).

Kwa mujibu wa Ripoti iliyotolewa juzi na Shirika la Ukaguzi wa Mahesabu la PwC, Jiji la Dar es Salaam pia lina sifa ya ukuaji wa kasi wa idadi ya watu kwa kuwa na alama 19 kati ya 20, ukuaji wa kundi la watu wenye kipato cha kati (alama 15 kati ya 20), huku likiboronga katika vipengele vya urahisi wa ufanyaji biashara (9), na mvuto wa uwekezaji wa kigeni (8).
Katika eneo hilo, jiji hilo ambalo ni kitovu cha biashara nchini, linafuatiwa na majiji ya Lusaka (Zambia), Nairobi (Kenya), Lagos (Nigeria), Accra (Ghana) na nafasi ya 10 katika kipengele hicho ikishikwa na Jiji la Cairo (Misri).
Katika nafasi ya jumla ya kifursa barani Afrika, Dar es Salaam limetupwa katika nafasi ya 15 nyuma ya majiji ya Nairobi, Kigali, na Kampala, katika nafasi ya 10.
Katika ripoti hiyo iitwayo ‘Ndani ya Afrika: Majiji yenye fursa’ na kusainiwa na Paul Monekosso Cleal, Pierre-Antoine Balu na Jonathan Cawood, PwC katika fursa za jumla ilichambua hali ya miundombinu, nguvukazi, uchumi na jamii pamoja na sifa za watu wa majiji husika.
“Jambo la msingi ni kwamba maendeleo ni suala la hatua mbalimbali katika kipindi fulani. Lakini hatua hizo ni lazima ziratibiwe vizuri na kutekelezwa kwa wakati.
“Tunaamini kuwa uchambuzi ulioanishwa katika ripoti yetu utawapa fursa watunga sera, wafanyabiashara na wawekezaji kuendelea na mikakati yao ya kimaendeleo yenye tija katika majiji husika,” ilisema sehemu ya ripoti hiyo.
Ripoti hiyo ilieleza kuwa kuwapo kwa fursa hizo hakumaanishi hakuna changamoto katika majiji hayo na kwamba kila jiji lina mazuri yake na mabaya yake na kuongeza kuwa uchambuzi wa namna hiyo ni kazi endelevu

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!