Thursday 19 March 2015

CHEKA AANZA KUFYEKA MAJANI



Bondia Francis Cheka ameanza kutumikia adhabu yake ya kifungo cha nje kwa kufyeka majani.



 
Cheka alifanya kazi hiyo jana ikiwa ni siku moja tu baada ya kuchiwa kutoka jela kwa ajili ya kuanza kutumikia kifungo cha nje mwaka mmoja nje ambacho amepewa baada ya kuonyesha tabia njema gerezani na sasa atatumikia kwa kufanya kazi za kijamii.
 
Bondia huyo anayekubalika zaidi nchini hivi sasa, Februari 2, mwaka huu alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani na kulipa faini ya Sh. milioni moja mara atakapotoka gerezani huu kwa kumpiga Bahati Kibanda  aliyekuwa meneja wa baa yake.
 
Ofisa Ustawi wa Jamii, Yusufu Fonera, alisema kuwa Cheka ametoka gerezani kwa mujibu wa Sheria ya Magereza Namba 34 ya mwaka 1967 kifungu cha 51 kilichofanyiwa marekebisho ya sheria namba 9 mwaka 2002 kinachompa uwezo mkuu wa gereza kuomba kupunguzwa kwa adhabu ya mfungwa.
 
Kifungu hicho cha sheria kinamruhushu mkuu wa gereza kuiomba ofisi ya ustawi wa jamii kubadilisha au kupungaza adhabu kwa mfungwa endapo itaridhika na tabia ya mfungwa huyo akiwa gerezani.
 
Cheka ni miongoni wa watu 50 walioombewa na mkuu wa gereza kupunguziwa adhabu baada ya kuonyesha tabia nzuri ya uadilifu gerezani.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!