CHANZO CHA MOTO KIKIWA NI MAFUTA YALIYOKUWA KATIKA MTALO HUU AMBAPO MAMA MMOJA ALIENDA NA KIBATARI ILI KUANGALIA KAMA YALIKUWA NI MAFUTA AU MAJISEHEMU ILIPOTOKEA AJALI YA GALI T821ARF KATIKA KIJIJI CHA ISONGOLE (NO ONE) NA KUSABABISHA WATU WATATU KUFA NA KUMI NA NNE WAKIWA KUJERUHIWA MMOJA WA MAJERUHI WA AJALI YA MOTO AKIUGULIA VIDONDA NA MAUMIVU YA MOTOKUSHOTO DEREVA WA GARI LILILOPATA AJALI ZAWADI NYATO AKIWA NA MKEWAKE NA KAKA YAKE KATIKA HOSPITAL YA IGOGWE TUKUYU AKIWASIMULIA JINSI AJALI ILIVYOTOKEA KUWA “NILIPOKUWA NASHUKA MILIMA YA ISONGOLE KARIBU NA KABURI PALE JUU NIKAONA TAA ZA UPEPO WA GALI LANGU HAZIWAKI NA NIKAONA GALI HALIKAMATI BREKI HIVYO KWAKUWA NILIKUWA NA MZIGO MZITO GALI LIKANISHINDA NA SASA NAJIKUTA NIPO HOSPITALI ILA HADI HAPA SIJAELEWA KILICHOTOKEAMMOJA WA WAGOJWA WALIO KATIKA HALI MBAYA KATIKA HOSPITAL YA IGOGWE WAKIENDELEA NA MATIBABU
……………………………………………………………………………
Watu watatu wamefariki dunia kwa ajari ya moto akiwemo utingo wa gari hilo aliyefia hospitali kwa kuvuja damu nyingi na watu kumi na nne kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Igogwe ambapo watatu wamethibitishwa na Daktari kuwa hali zao ni mbaya baaada ya gari aina ya Scania lenye namba za usajiri T821ARF mali ya kampuni ya Irasi likiwa limebeba mafuta ya petrol, kuacha njia na kupinduka muda ya saa tatu usiku eneo la kijiji cha Isongole (Nomber One )kata ya Isionje .
Moto huo uliosababishwa na mwanamke aliekuwa na kibatari kwenda kumulika mafuta katika mfereji wa maji uliopo eneo la tukio kwa kibatari chake ili ajue kama yale ni mafuta au maji kitendo kilichosababisa moto kuwaka kufuata mafuta yaliyo kuwa yakimwagika mpaka eneo gari lilipoanguka hivyo kusababisha watu mifugo na mashamba kushika moto.
Moja wa shuhuda wa tukio aliyejitambulisha kwa jina moja la Matola amesema kwamba gari lilianguka mida ya saa tatu usiku ndipo wananchi walikimbilia kuchota mafuta na dereva na baadhi ya wakazi aliwakataza kusogea eneo hilo na kuwataka wawasaidie kutoka eneo hilo na baada ya mda kidogo wao kutolewa ndipo moto ulilipuka kutoka katika mfereji wa maji na kusambaa kufuata mtiririko wa mafuta hadi kufika kwenye gari.
Bwana Matola alifafanua kuwa“ Tunashukuru moto uliwahi kuwaka kabla ya watu kujaa hata hivyo baadhi ya wenyeji wa eneo hilo walijitahidi kuzuia watu wasichote mafuta lakini wengine hawakuweza kuwasikiliza wakizani kwamba watapata mafuta kama ilivokuwa juzi (siku tatu nyuma )baada ya gari la mafuta ya dizeli kuanguka na wao kuchota mafuta mengi na kuuza lita ishirini kwa shilingi elfu saba tu, hadi alipotokea mama moja ambae ni moja wa waliofariki kuja na kibatari kumulika mferejini ili kujua kama yale ni mafuta au maji na ndipo mafuta yakashika moto.”
Dereva wa gari hilo Zawadi nyato aliyekimbizwa hospitali ya igogwe baada ya kupata ajari amesema kuwa alipokuwa kwenye mlima anashuka taa ya upepo iliwaka kuashiria hakuna upepo na kwa sababu alikuwa amebeba mzigo mzito gari likamshinda na kujikuta yuko hospitalini bila kujua kilichoendelea hapo.
Nae mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Chrispin Meela amefika eneo la tukio kutoa pole na rambi rambi kwa wakazi wa eneo hilo na kuwakumbusha kuwa wawe makini na vitu vya hatari kama hivi kwani tukio kama hili liliwahi kutokea katika mtaa huo huo na kusababisah vifo vya watu wengi lakini bado wanarudia kitendo kama hicho. Hivyo amewataka watu wabadilike na wajifunze kupitia matukio yaliyopita.
Ajali ya moto kama hii iliwahi kutokea miaka ya 1990 katika kata hiyohiyo ya Isionje mita chache kutoka ilipotokea ajali hii ya leo na kuuwa watu wengi waliozikwa kwa pamoja katika eneo hilo kwani walishindwa kutambulika na ndugu zao na kijeruhi mamia ya watu.
Kwa hisani ya
TUMAIN OBEL
KINGO TANZANIA
Rungwe
No comments:
Post a Comment