Timu ya taifa ya Ivory Coast imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuifunga Ghana kwa mikwaju ya penati .
Timu hizo mbili zilimaliza muda wa kawaida wa dakika 90 zikiwa hazijafungana hali iliyolazimu kuongezwa kwa dakika 30 za nyongeza.
Dakika hizo ziliisha kwa timu hizo kushindwa kufungana hali iliyolazimu mikwaju ya penati kupigwa ili kumpata Bingwa.
Ivory Coast ilifanikiwa kushinda baada ya kufunga penati 9-8 .
No comments:
Post a Comment