Tuesday, 20 January 2015

WATU AROBAINI WANUSURIKA KUFA BAADA YA DALDALA KUGONGANA NA LORI TEGETA

Zaidi ya watu arobaini wamenusurika kifo huku mmoja akikatika viungo vya  miguu na wengine kujeruhika vibaya baada ya lori  moja lilionekana kuwa ni la jeshi kugongana uso kwa uso na gari la abiria aina ya COSTA la ubungo Tegeta eneo la Tegeta jijini Dar es salaam.



ITV imeshuhudia tukio hilo lililovuta hisia za mamia ya wakazi wa Tegeta huku baadhi ya mafundi gerejji wa Tegeta wakijaribu kutumia vifaa maalumu kukata mabati ya magari kwa nia ya kunasua baadhi ya majeruhi walionasa ndani ya COASTA hiyo kusuru abiria walioonekana kunasa katika vyuma vya magari hayo baadhi ya wamashuhuda na Dereva wa COSTA pamoja na kuomba eneo la kibaoni kuweka njia ya mzunguko maarufu kama ROUND ABOUT kwa lengo la kuepusha madereva wanao lazimika kugeuza kwa dharura katika njia kuu maarufu kama UTAN kutokana na njia hiyo kukosa fursa ya kugeuza endapo kuna ulazima wa kufanya hivyo pia wamemtupia lawama Dereva wa Lori kama msababisha ajali kwa kukosa hekima ya kuchukua tahadhari kabla ya kufanya hivyo.
 
Kamanda wa polisi mkoa kipolisi kinondoni  Kamilius wambura amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akieleza kutoa taarifa mara baada ya uchunguzi kufanyika.

CHANZO: ITV

1 comment:

Anonymous said...

maiko johny10:53


1


mungu wangu

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!