Wednesday, 28 January 2015

MSIBA UK.


Asalam Aleykum, tumepata msiba mkubwa, ndugu yetu mwenzetu, ustadh wetu na rafiki wa tangu na tangu, mfuasi madhubuti wa Ahlulbayt (as) ustadh Khatibu Musa Irovya ameaga dunia tarehe 22/01/2015 nyumbani kwake South London baada ya kuugua kwa muda.


Tunapenda kuwajulisha kuwa maziko ya ustadh khatibu Musa yatakuwa kesho kutwa, siku ya alkhamis 29/1/2015 mara tu baada ya swala ya adhuhuri. Maandalizi pamoja na swala yatafanyika katika msikiti ulioko makaburini. Maziko yatakuwa katika makaburi ya Gardens of peace, huko HAINAULT, Anuani ya makaburini ni ELMBRIDGE Road, ILFORD, IG6 3SW. Kina mama watakusanyika katika ukumbi wa MCE (Muslim Community of Essex). Sura al fatiha kwa ajili ya marehemu.
Tafadhali tushirikiane na tuwajulishe jamaa wote na tuwahimize wenye fursa waje mazikoni! Shukran..

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!