Wednesday 3 December 2014

WATOTO NI TAIFA LA KESHO SOTE KWA UJUMLA TUSAIDIANE KUPUNGUZA TATIZO LA WATOTO WA MITAANI







 Wananchi pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali nchini tulitambue hili, kuwa watoto ni taifa la leo na kesho hivyo wanapaswa kuendelezwa ,kulindwa kushirikishwa na kutobaguliwa.

Shida na mateso wanayoyapata watoto waishio katika mazingira hatarishi na wale wa mitaani ni vigumu kueleza. Watoto hawa hawajui leo au kesho watakula nini ,hakuna anayeangaika kuwatafutia chakula ,wanapolala na njaa hakuna wa kumlilia na wakiumwa hakuna wa kumweleza hivyo huendelea na maisha yao hadi wanapopata nafuu au kupona kabisa.




Hata hivyo wakazi wa jiji la DSM wamedai kuwa tatizo la ongezeko la watoto wanaoishi mitaani linaendelea kuwa sugu nchini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya familia nyingi kutokuwa na malezi bora kwa watoto na tabia iliyoanza kujitokeza siku hizi ya ndugu kuacha kuleleana watoto 




 Ukweli na kwamba ,watoto hawa hujisikia wapweke kutokana na jamii kubwa kuwakataa na kuwaweka katika fungu tofauti. Jambo la kusikitisha ,idadi kubwa ya watoto umri wao unaanza miaka miwili hadi kumi ambao kimsingi hawajui kujitegemea ,njaa ikiuma wanalia tu na kushindwa kujieleza. Kitanda chao ni barabarani na wengine mitaroni ,baridi yote ya usiku na jua la mchana ni lao ,hawajui kubadilisha nguo,zile walizovaa wiki iliyopita hadi leo hazijatoka mwilini,  Tumezowea kuwaona watoto wenye wazazi wakitoka nyumbani asubuhi na kurudi majumbani mwao jioni .Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi hawana pa kwenda ,popote wanalala.  Jamii imesahau kuwa watoto hawa ni sawa na wao ,wanasikia njaa ,baridi na maumivu sawa na wenzao lakini nani anashughulika nao?


Hatua za haraka zinahitajika ili kupunguza au kumaliza tatizo la watoto wa mitaani  na yatima kwa kuwaunganisha na walezi pamoja na ndugu zao ambao tunaamini wapi.
      Umefika wakati wa serikali kuratibu nguvu za NGOs kwa kuhakikisha mashirika hayo,jamii na wao wenyewe wanachukua hatua stahiki  kuhakikisha tatizo hilo nchini linakwisha... 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!