Mara nyingi watu hutumia siagi ya karanga (peanut butter) kwenye mkate au kama kionjo kwenye mboga ya majani.
Leo nitakufundisha kutumia siagi ya karanga ,matunda na mboga za majani kuandaa vitafunwa (snacks).
Vitafunwa hivi ni namna nyingine nzuri yakula matunda na mboga zamajani fresh,ni vitafunwa ambavyo hushibisha kwa haraka na kwamuda mrefu.Ni rahisi kuandaa huitaji kupika chochote.
Mahitaji
- Beat roots (viazi vyekundu),menya kata vipande vyembamba
- Nanasi,menya kata vipande vinene
- Ndizi mbivu ,menya kata vipande vinene
- Limao,kamua upate maji yake
- Majani ya giligiliani,osha kata vipande vidogo vidogo
- Siagi yakaranga (peanut butter)
- Mdalasini (tumia yaunga
- tangawizi (tumia yaunga)
- Tooth picks
Njia
Nanasi na Beatroot
1.Chukua kipande cha nanasi,pakaa siagi ya karanga (weka nyingi),weka giligiliani kiasi juu yake ,nyunyuzia tangawizi kidogo juu ya giligiliani,kisha weka kipande cha beat root (viazi vyekundu).chomeka toothpick katikati .Fanya hivi adi upate idadi upendayo
- Unapochomeka toothpick hakikisha imefika chini ,kwani utatumia toothpick hiyo kunyanyua na kula kitafunywa hiki,tizama mfano katika picha
2.Panga vitafunwa hivi vizuri kwenye sahani au bakuli,funika kisha weka kwenye friji au friza ili viwe baridi au vigande.unaweza kula vikiwa baridi au vikiwa vimeganda.pia unaweza kula bila kuweka frijini.Unaweza hifadhi frijini kwaajili ya matumizi ya wakati mwingine.
Ndizi na Limao
1.Chukua kipande cha ndizi mbivu,pakaa siagi yakaranga,kisha nyunyuzia mdalasini juu yake,weka ndizi nyingine juu yake,kisha nyunyuzia maji yalimoa juu ya ndizi.chomeka toothpick katikati ukipenda
Ni muhim sana kunyunyuzia limao juu ya ndizi ili kuzuia ndizi kubadilika rangi kwa haraka nakua nyeusi.
2.weka kitafunwa hiki kwenye friza ili kigande kama barafu.Toa kwenye friza acha kiyeyuke kidogo pale unapotaka kula.Usihifadhi kitafunywa hiki kwenye friji kwa muda mrefu kwani kitabadilika rangi nakua cheusi.
Tumia vitafunwa hivi wakati wowote unapohisi njaa badala yakunywa vitu kama soda au kula biskuti.
Vitafunwa hivi hupendwa sana na watoto na unaweza vitumia hata kwenye sherehe za watoto kama birthdays.
SPECIAL THANKS TO TOLLYS KITCHEN.
No comments:
Post a Comment