Friday 12 December 2014

VAN VICKER NA WEMA SEPETU WAKUTANA

Kama ulibahatika kuona picha katika mitandao ya kijamii ikimwonyesha Miss Tanzania 2006 ambaye pia ni mwigizaji, Wema Sepetu akiwa na nyota wa filamu kutoka Ghana, Van Vicker wawili hao wapo katika matayarisho ya filamu mpya imedhibitishwa.

Mkali huyo wa filamu Afrika Magharibi alithibitisha hilo, kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter huku akimsifia mlimbwende huyo kwamba ni mwigizaji mzuri.
“Kitu changu kingine kikubwa, nimefurahia muunganiko baina ya Ghana na Tanzania, ni siku ya kwanza lakini nimefurahishwa na namna tulivyoweza kuifanya kazi hii kwani unajua nini unakitaka. Nimefarijika kufanya kazi na wewe, katika filamu hii itakayojulikana kwa jina la ‘Day After Death’, mhusika mkuu ni Wema Sepetu na mimi,” aliandika katika mtandao wa huo alfajiri ya jana.
Van Vicker aliweka wazi kuwa filamu hiyo aliyoiongoza, ilimpa wakati mgumu lakini anafurahia changamoto alizopewa na mlimbwende huyo.
“Katika filamu hii watazamaji pia watawaona mabinti zangu wawili ambao wameigiza ndani yake.”
Meneja wa Wema, Martin alisema kuna kazi kadhaa zinazofanywa chini ya Kampuni ya Endless Fame na kampuni ya Van Vicker kwa sasa.
“Van Vicker kupitia kampuni yake ya Sky + Orange Productions ambayo yeye ni mkurugenzi mkuu na Wema kupitia Endless Fame akiwa mkurugenzi mkuu pia, wameungana kufanya mradi na tayari wameshafika nchini Ghana kwa ajili ya kukamilisha kazi hizo,” alisema Kadinda na kuongeza: “Huu ni mradi mkubwa ambao wanauandaa utakaojumuisha kampuni hizi mbili, kwa hiyo mashabiki wake wategemee makubwa inaweza kuwa filamu au vinginevyo wasubiri matokeo, Wema ameongozana na Petitman mmoja kati ya wafanyakazi wa kampuni.”
Wema aliandika katika ukurasa wake wa Instagram: “Tupo katika matayarisho.”

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!