Saturday, 6 December 2014

SARATANI (CANCER) NI NINI?



Cancer
Mwili wa binadamu umeundwa kwa chembe hai ndogo ndogo sana, zinaitwa cells. Ziko cells za aina mbalimbali, ambazo hujikusanya na kutegeneza tissues. Nazo zinapokuwa nyingi hutengeneza viungo mbalimbali katika mwili wa binadamu mfano ini, figo, jicho, ngozi, moyo, ubongo,n.k


Kwa kuwa hizi cells zinaishi, basi huchakaa, huharibika na pia hufa.. Zinapokufa, huzaliwa nyingine na kuriplesi zile mbovu zilokufa, ili mwili uendelee kuishi.
Cell inapoharibiwa, huwa inajaribu kujitengeneza, au kujizalisha upya. Hili suala lazina kuwe na kidhibiti au control mechanism. Vinginevyo cells zitaongezeka bila mpangilio, na pengine bila kufanya kazi yake ya awali. Hizi ndo zinaitwa cancer cells. Ni cells zinazojiotea bila mpango, kwa spidi kali zaidi, wala hazifanyi kazi za asili za kumsaidia mwili, bali hudhuru mwili.
Kuna cancer za aina nyingi sana, zingine huua katika muda mfupi, zingine huchukua muda mrefu, zingine hutibika, zingine hazitibiki, zingine hujitokeza haraka, zingine huchelewa.
Sababu za cancer ni nyingi, zingine sababu moja tu hupelekea cancer, zingine ni mjumuiko wa sababu zaidi ya moja.
Miongoni mwao;
- Za urithi katika familia
- Mionzi ya jua mikali.
- Makemikali ya viwandani.
- Uchimbaji madini mf uranium, asbestos, mercury, lead
- Uchimbaji mafuta, gesi
- Utengenezaji sumu za kuulia wadudu
- Mionzi ya X-rays
- Madawa ya kubabua ngozi, mkorogo.
- Mashambulizi ya virusi
- Baadhi ya dawa kali za kutumia binadamu.
- Tumbaku, sigara, ugoro, pariki, kubeli, tambuu, n.k
- Kuishi karibu na takataka za sumu za kiwandani n.k
Tiba
Kama nilivyoeleza mwanzo, zingine hutibika zikigundulika na mapema, zingine hazitibiki. Kuna tiba za ;
- operesheni,
- mionzi (radiotherapi) na
- dawa (kemotherapi)

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!