Tuesday 9 December 2014

MAPENZI YA JINSIA MOJA MARUFUKU MISRI

Viongozi wa juu nchini Misri wametoa tamko baada ya uvamizi wakati wa usiku katika nyumba inayotumiwa na wapenziu wa jinsia moja kuoga pamoja mjini Cairo

Wanaume nane walikamatwa na sasa wanakabiliwa na kosa la kufanyia mzaha dini kosa ambalo limekuwa likituhumiwa watu wanaokamatwa kwa kushukiwa kujihusisha na vitendo vya wapenzi wa jinsia moja.
Mahaba ya jinsia moja hayajapigwa marufuku nchini Misri,lakini watu wanaoshukiwa kuwa si 'rizki' huweza kukabiliwa na mashtaka ya mzaha katika dini na ufisadi.
Wanaume hao nane walitiwa korokoroni siku za karibuni kwa kukiuka maadili ya umma na hii ni baada ya video moja kuachiliwa ikionyesha ndoa iliyofungwa ya wapenzi wa jinsia moja na kuanikwa katika mitandao ya kijamii.

1 comment:

Anonymous said...

Eeeh Mola inusuru dunia na nchi yetu Tz kujihusisha na huo uovu.

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!