Friday 5 December 2014

MAISHA YA ASKOFU BILLIONEA

Mbali ya kuwa na chopa iliyokuwa ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi karibuni, askofu huyo alikuwa na msururu wa magari yenye thamani kubwa yanayomfanya kutajwa kuwa tajiri kuliko maaskofu wengine wanatoa huduma katika makanisa ya kiroho Tanzania.


 Akiwa Karatu, mbali na ulinzi binafsi, Geordavie alikuwa akilindwa na askari wa jeshi la polisi, askari kanzu, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa usalama barabarani.Mbali na askari hao wa serikali ambao wamekuwa wakimlinda kila anapofanya mikutano yake, pia Geordavie analindwa na askari wake binafsi hali iliyowafanya baadhi ya watu kuamini kuwa ulinzi wake ni kama ule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’. “Sijawahi kumuona JK akilindwa na chopa lakini mtumishi wa Mungu Geordavie analindwa na ndege katika msafara wake! Hii ni mara yangu ya kwanza kuona,” alisema muumini mmoja ambaye hakupenda kutajwa gazetini.
Hata hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji utajiri wa askofu huyo kutokana na fedha nyingi anazozitumia anapofanya mikutano katika sehemu mbalimbali jijini Arusha. “Tunajua kuwa ni tajiri, lakini anapata wapi fedha za kutumia hivi?” alihoji muumini aliyejitambulisha kwa jina moja la Julius ambaye naye alihudhuria mkutano wa askofu huyo anayetumia kaulimbiu ya Ngurumo ya Upako katika kutoa huduma yake.

1 comment:

Anonymous said...


HII NAYO SHIDA!!

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!