Friday, 5 December 2014

AHSANTE MDAU WA SOPHIEMBEYU BLOG KWA ZAWADI YA DAGAA!




Jamani wadau nimeletewa dagaa na mdau wa sophiembeyu blog, toka Canada, sasa hizi dagaa ni kama za kigoma kabisa! tena hazina mchanga hata kidogo!mambo ya diet yamesimama kwa muda ni mwendo wa Ugali na dagaa,Nashukuru saaana Ankal Bilal !
KWA WALE WASIOJUA KUPIKA DAGAA WA MAWESE KARIBU UJIUNGE NAMI MAELEKEZO YAKO CHINI HAPO!





kuzitayarisha hizo dagaa,kwanza chukuwa frying pan na uzitupie ndani yake dagaa unazokusudia kuzipika bila ya kuzitia ktk maji ,zikaange mpaka zibadilike rangi kidogo angalia usiziunguze na zikiwa tayari zitoe na weka pembeni usizioshe na maji ya aina yeyote wala usizitoe vichwa then chukuwa sufuria moja ndogo na kata kata vitunguu na tomatoes halafu tia vitunguu na nyanya ndani ya sufuria washa jiko na hapo hapo tia mawese ndani ya hilo sufuria na uanze kuvikaanga vitunguu na tomatoes pamoja mpaka ukiona zinabadilika rangi zinaanza kuiva zitupie dagaa ndani ya sufuria ukaangie pamoja na hivyo vitunguu na nyanya kwa pamoja na uongeze mafuta ya mawese kidogo na kama una vergie kidogo ka mchicha au mboga ya collard tupia ndani changanya pamoja na funika sufuria mpaka ziwive usikose wakati wa kuanza kuzikaanga na vitunguu na nyanya weka kipande nusu cha magi ili chumvi ichanganyike,usiweke piece moja kubwa chumvi itazidi na pia tumia lemon au piece moja ya lime na kama wewe ni mpenzi wa pilipili ka mimi tumia fresh pilipili ili kuongeza ladha baada ya kuzifunika for sometime,dagaa tayari pika ugali wako and bon pettit! enjoy your meal.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!