Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab wamekiri kuhusika na mauaji hayo.
Mkuu wa Polisi eneo hilo, amesema bado wanafuatilia tukio hilo.
Katika tukio lingine, mtu mmoja ameripotiwa kuuawa nchini Kenya kufuatia mlipuko katika klabu moja ya usiku katika mji wa Wajir kaskazini mwa Kenya.
Washambuliaji hao walitumia magruneti na silaha nyingine za kijeshi kufanya shambulio hilo.Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi wa Wajir, Frederick Sishia, shambulio hilo limefanyika saa mbili usiku na kuua mtu mmoja na watu wengine wanne wamejeruhiwa.
Wiki iliyopita watu wengi waliuawa eneo la Mandera kaskazini mwa Kenya.
Kenya imejikuta ikilengwa na mashambulio ya kigaidi tangu majeshi yake yapelekwe nchini Somalia kukabiliana na wapiganaji wa Al Shabab. Mbali na miji ya kaskazini mwa Kenya kushambuliwa kila mara, miji mikubwa nchini humo ya Nairobi na Mombasa imekuwa ikilengwa na mashambulio ya kigaidi.
No comments:
Post a Comment