Ripoti iliyokuwa ikisubiriwa na wananchi kuhusu ukweli wa uchotaji wa mamilioni ya fedha kutoka akaunti ya ESCROW ya Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha kashfa miongoni mwa wanasiasa na maafisa wa serikali na majaji imejadiliwa katika bunge.
Ripoti ya kamati ya PAC imefuatia kuwasilishwa kwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini humo, TAKUKURU, zilizowasilishwa bungeni hapo.
Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya bunge, taarifa ya PAC itawasilishwa leo jioni kuanzia saa kumi na moja jioni na kujadiliwa kwa siku mbili ujadiliwa kwa siku mbili. Hata hivyo kabla ya kuwasilishwa kwa taarifa hiyo, kumeibuka madai ya kuwepo zuio la Mahakama Kuu kuhusu kujadiliwa kwa ripoti ya PAC.
Naye mwenyekiti wa bunge hilo Mussa Zungu Azan anawahakikishia wabunge kuwa ripoti hiyo itawasilishwa kama ilivyopangwa.
No comments:
Post a Comment