Jeshi la polisi Zanzibar linawashikilia raia wawili wa kigeni baada ya kukutwa na silaha na risasi kinyume na sheria huku mmoja ya raia huyo wa ufaransa amewajeruhi watu sita kwa kuwapiga risasi kutokana na mgogoro wa umiliki wa hoteli.Akithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao katika matukio tofauti Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar Kamishna Msaidizi Mwandamizi Salum Msangi amewataja watuhumiwa hao ambao watafukishwa mahakamani kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria ni Artur Miarka ambaye alikutwa na bunduki na risasi aina ya Shotgun.
Aidha Kamishna Msangi ametoa wiki moja kwa wageni wakiwemo wawekezaji na wazalendo ambao wanamiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha kabla ya jeshi hilo kuanza oparesheni maalum ya kuzisaka silaha kutokana na kuwepo kwa ongezeko la watu kuwa na silaha Zanzibar.
Hili ni tukio la Nne katika kipindi kifupi kwa jeshi la polisi kufanikiwa kuwakamata watu wenye silaha na wengine kukutwa na mabomu kisiwani Zanzibar hali inayowafanya wananchi wengi wahoji hali ya usalama na vipi silaha hizo zinapita bila ya kugundulika
No comments:
Post a Comment