Saturday, 29 November 2014
MTAMBO WA GESI YA NYUMBANI KUJENGWA KWA MIAKA 7
UJENZI wa mtambo wa kuchakata gesi asilia kwa ajili ya matumizi mbalimbali (LNG) mjini Mtwara, unatarajiwa kuchukua miaka saba. Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Statoil Tanzania, Thomas Mannes amesema kuwa, mambo yakienda kama yalivyopangwa, mtambo huo utakuwa tayari kwa uchakataji kati ya mwaka 2022 na 2023.
Akizungumza na viongozi wa dini wa Tanzania waliotembelea mtambo wa uchakataji gesi wa Statoil uliopo Karsto, Mannes amesema kuwa mradi huo mkubwa utagharimu mabilioni ya dola za Marekani.
“Tunakadiria itachukua kama miaka saba, mmoja kwa utafiti wa eneo kujua uimara wake kiufundi, miaka miwili ya utafiti wa kiuhandisi na michoro na miaka minne ya ujenzi wenyewe,” alisema.
Kwa mujibu wa Mannes, tayari wameshapendekeza maeneo yanayofaa kwa ujenzi wa mtambo huo na hivi sasa wabia wa mradi wanateua timu ya pamoja itakayosimamia mradi huo.
Mradi huo utakuwa wa pamoja kati ya Shirika la Maendeleo ya Mafuta nchini (TPDC) na kampuni za Statoil, BG, ExxonMobil, Ophir na Pavilion.
Mradi huo utaenda sambamba na miradi mingine ya mafuta ya vitalu 1,3 na 4 inayoshirikisha TPDC, BG, Ophir na Pavilion na mradi wa gesi wa kitalu 2 wenye ubia kati ya TPDC, Statoil na ExxonMobil.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment