Friday, 28 November 2014

GHARAMA KUBWA KUTIBU MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TIKETI YA KIFO

Kuishi ni jambo moja. Kuishi maisha yenye afya njema ni kitu kingine.
Hakuna anayeweza kushuhudia juu ya ukweli huu zaidi ya wale wapatao adha itokanayo na  athari za magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni Shirika la Afya Duniani (WHO), idadi ya vifo vitokanavyo na magonjwa ya figo nchini Tanzania imefikia 4,533 sawa na asilimia 1.03  ya vifo vyote kwa jumla wakati kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa figo katika Tanzania imeripotiwa kuwa katika asilimia 14 .
Wakati huohuo, Taasisi ya Figo ya Taifa inaonyesha kuwa gharama za kusafisha damu kwa mgonjwa wa figo ni zaidi ya Sh4.5 milioni kwa wiki.
Matibabu ya kubadilisha figo nje ya nchi ni zaidi ya milioni 50.
Idadi kubwa ya Watanzania  watu wazima na watoto wasio na hatia  ndio  waathirika  wanaopata mateso makubwa  kutokana na  aina mbalimbali ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ikiwa ni pamoja na magonjwa ya moyo, ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya figo, mifumo ya neva, uti wa mgongo na magonjwa mengine yanayohusiana na haya.
Kwa bahati mbaya, licha ya mipango mikakati ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza nchini, Watanzania wengi bado wanaathirika na kupoteza maisha kutokana na magonjwa haya.
Sababu kuu ya vifo kwa  wagonjwa hawa ni kushindwa kwa figo na mishipa ya  moyo au madhara yatokanayo na matatizo hayo.
Kujenga mipango endelevu  ya matibabu kwa wagonjwa wa figo, moyo, kisukari, mfumo wa mkojo, mfumo wa neva na uti wa mgongo  inaendelea kuwa changamoto nchini Tanzania.
Kama sehemu ya ushirikiano na jitihada za pamoja  katika kutokomeza  magonjwa yasiyo ya kuambukiza katika kiwango cha kimataifa, wiki iliyopita madaktari mashuhuri  kutoka Hospitali ya Apollo yenye makao makuu nchini India mjini Hyderabad, wamechukua hatua ya kufanya kliniki ya siku nne kwa lengo la kupitia upya kesi za wagonjwa mbalimbali, kutoa ushauri na matibabu kwa wagonjwa hao, na kufuatilia wagonjwa wa Kitanzania waliowahi kuenda Hospitali ya Apollo nchini India kwa ajili ya matibabu.
Baada ya kufanya kazi kwa karibu  na  madaktari  wenzao wa Tanzania katika Hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam, madaktari hao si tu walitoa ushauri na tiba kwa  wagonjwa juu ya maradhi yao bali walikuwa na uwezo wa kushiriki katika ufahamu juu ya hali ya  magonjwa hayo nchini Tanzania.
Katika kuchambua juu ya idadi ya wagonjwa wanaosafiri kutafuta matibabu nje ya nchi.
 Mtaalamu wa mfumo wa mkojo na njia ya uzazi,(Neurologist) Dk.Rajagopal Krishnan anasema kuwa kuna idadi kubwa ya wagonjwa wa kimataifa ambao hutembelea vituo vyao kila mwaka.
Zaidi ya  asilimia 30 hadi 40 ya wagonjwa wanaohudhuria Hospitali ya  Apollo wanatoka barani Afrika na idadi kubwa ya wagonjwa hao ni kutoka Tanzania.
Kutokana na gharama zitokanazo na  safari kwa ajili ya matibabu nje ya nchi, wagonjwa wengi hawawezi kumudu kurudi kwa ajili  utaratibu wa kufuatiliwa maendeleo ya hali ya afya zao na kuwategemea madaktari wa ndani. 
Kliniki hiyo si tu iliruhusu kuangalia  kesi za wagonjwa wapya, lakini pia ilikuwa ni fursa kwa madaktari kukutana na baadhi ya wagonjwa  wao waliopo nchini Tanzania na  hivyo kuwasaidia katika kupunguza  gharama ya kurudi tena nchini  India .
Dk Phillip Robert Hiza ni miongoni mwa wagonjwa waliopata nafasi ya kuonana na madaktari hawa bingwa  kutoka Apollo.
Kesi yake ilikuwa maalumu kwa kuwa aligundulika na  ugonjwa wa saratani  ujulikanao kama ‘Multiple Myeloma’. Katika kushauriana na madaktari nchini, ugonjwa huo uligundulika kutokuwa na  tiba. Alipelekwa Hospitali ya Apollo, Hyderabad (India) kwa ajili ya matibabu kwa kipindi cha miezi mitano.
Katika kipindi hiki alihudumiwa  na Dr Sanjay Maitra mmoja wa wataalamu bingwa wa magonjwa ya figo  kutoka Apollo.
Katika mahojiano maalumu na Dk Sanjay Maitra, anaelezea kuwa hii ni ziara yake ya tano  Tanzania  na kuelezea muitikio wa Watanzania katika kliniki hiyo.
Anasema alilenga zaidi juu ya wale walio na matatizo ya figo. Daktari huyo alikuwa na uwezo wa kuona zaidi ya wagonjwa 25 katika kipindi hiki.
“Idadi kubwa ya Watanzania hawana ufahamu wa kutosha juu ya matatizo ya  figo. Uelewa huo mdogo kwa umma kuhusu ukali wa matatizo hayo umesababisha watu wengi kutojua jinsi magonjwa hayo yanavyoweza kusababisha madhara makubwa katika mifumo  mbalimbali ya mwili, mfano katika ubongo, moyo, figo, macho na mishipa ya damu “, anasema.
Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Shirika la Afya Duniani wa 2008-2013  wa kukinga na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza, unatoa wito kwa nchi zinazojiweza kushirikiana na kutoa msaada kwa nchi zenye uwezo wa  chini na kati ya kwa ajili ya programu ya kupambana na magonjwa yasiyo ya  kuambukiza.
 Mtaalamu wa magonjwa ya figo Dk Sanjay Maitra pamoja na kitengo cha Figo katika Hospitali ya Apollo hivi sasa  wanampatia mafunzo daktari wa Kitanzania katika hospitali yao
Mafunzo hayo ni kwa ajili kumsaidia daktari huyo kuwa na uwezo wa kutambua matatizo ya msingi yanayohusiana na figo, kushindwa kwa figo na kutoa matibabu kwa watu wenye matatizo ya figo.
MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!