Monday, 15 September 2014

WANAUME ACHENI TABIA YA KUPIGA WANAWAKE! "CHAZ BABA" AMPIGA MKE WAKE NA KUMJERUHI!!

PREZIDAA wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Mbwana ‘Chaz Baba’ anadaiwa nusura amtoe roho mkewe wa ndoa, Rehema Sospeter Marwa baada ya kumpiga  na kitu kizito kichwani mpaka kushonwa nyuzi ishirini.
Mke wa ndoa wa 'Chaz Baba', Rehema Sospeter Marwa akiwa na majereha kichwani.


MANENO YA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo karibu na wanafamilia hao (jina limehifadhiwa), usiku wa Alhamisi iliyopita, kikiwa maeneo ya Kinondoni jijini Dar kilishuhudia ugomvi huo baada ya kwenda kuangalia nani anamshushia kipondo mwenzake.
Chanzo kilisema baada ya kufika, ndipo kiligundua kuwa, mwanamuziki huyo ndiye aliyekuwa akimpa kipondo mke wake.
“Dah! Kiukweli kile si kipigo cha kumpiga mke, hasira bwana ni kitu cha ajabu sana. Chaz anatakiwa kujiangalia sana,” kilidai chanzo hicho.
MKE AFUNGUKA ‘EI TU ZEDI’
Baada ya taarifa hiyo, juzi Ijumaa Wikienda lilimtafuta mwanamke huyo ili aeleze nini kilitokea hadi mumewe kutaka kumkatishia maisha.“Nakumbuka siku ya tukio nilikuwa supermarket maeneo ya Mwananyamala A (jijini Dar) nikinunua unga wa ulezi wa mtoto, ghafla Chaz alitokea, akaniamuru niingie kwenye gari alilokuwemo, tukaondoka kuelekea nyumbani.
Rehema Sospeter Marwa akionesha majeraha aliyoyapata mkononi.
“Tulipofika maeneo ya Kinondoni, pale Meridian ndipo niliposhtukia naanza kupigwa. Nakumbuka nilipigwa hadi nikaishiwa nguvu mpaka akatokea rafiki wa Chaz, Hassan Kisanora na kuniokoa, nikakimbilia nyumbani,” alisema mwanamke huyo.
CHAZ ATOWEKA, ARUDI NA SAMAKI MKUBWA
Akiendelea kuzungumza, mke huyo alisema: “Siku hiyo Chaz aliondoka na hakurudi nyumbani mpaka alfajiri. Aliporudi aliniambia amekuja na samaki mkubwa, yuko kwenye friji huku akisahau kuwa amenikosea na anatakiwa kuniomba msamaha.
“Sikumjibu, ndipo alipochukua kitu kizito na kunipiga nacho kichwani, baada ya hapo damu nyingi zikaanza kunitoka hadi puani, niliishiwa nguvu na kupoteza fahamu.”
“Nilipokuja kuzinduka nilikuwa hospitali kwa Dk. Mvungi, Kinondoni. Licha ya kwamba nampenda sana lakini alitaka kuniua, hata sijui kisa.”
Majeraha aliyoyapata baada ya kipigo kutoka kwa mume wake.
MADAI YA KUSHANGAZA; NDANI YA MIEZI TISA KICHAPO MARA 16
Katika kuweka mambo zaidi hadharani, mwanamke huyo aliyebahatika kupata mtoto mmoja na mumewe, alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, tangu afunge ndoa na Chaz miezi tisa iliyopita, ameshachezea kichapo mara kumi na sita hivyo amechoka kufanywa ngoma.“Nimechoka kufanywa ngoma na Chaz, ndoa ina miezi tisa tu nishapigwa mara kumi na sita kati ya hizo nimezimia mara saba kama vipi bora afanye utaratibu anirudishe kwetu,” alimalizia kusema.
CHAZ BABA, IJUMAA WIKIENDA
Baada ya kupata maelezo ya mke, Ijumaa Wikienda lilimsaka kwa njia ya simu Chaz mwenyewe ili azungumzie ishu hiyo ya mkewe kudai alimpiga ambapo alipopatikana alifunguka hivi:
“Ni wivu tu kaka! Unajua mke wangu ana wivu mkali sana, alianza kunipiga yeye mimi ndiyo nikamrudishia, hakukuwa na sababu nyingine yoyote zaidi ya wivu,” alisema Chaz bila kufafanua.
SERIKALI YALAZIMISHA WATU KUFANYA MAZOEZI.
Serikali kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) imewalazimisha watu kufanya mazoezi ya lazima baada ya kufunga kituo cha daladala cha Mwenge jijini Dar.
'Chaz baba' akiwa na mke kanisani siku ya ndoa yao.
Gazeti hili limekuwa likishuhudia umati wa watu asubuhi kati ya saa 1:00 na 2:00 wakitembea kutoka Makumbusho hadi Mwenge, hali iliyotafsiriwa kuwa serikali imewalazimisha kufanya mazoezi bila hiyari yao.
 Wakizungumzia hilo, baadhi ya raia wanaofanya kazi maeneo ya Mwenge na Mikocheni eneo la viwanda, wamesema baada ya kufungwa kwa kituo hicho, wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu asubuhi hivyo kuwafanya wanapofika maeneo yao ya kazi wawe wametoka jasho sana.
“Unajua asilimia kubwa ya tuliokuwa tunashuka Mwenge ni wa kipato cha chini, sasa baada ya kuhamishiwa Makumbusho, tunalazimika kutembea hadi Mwenge. “Tunachukulia kama ni mazoezi kwani baadhi tangu kuhamishwa kwa kituo hicho sasa hivi vitambi vimepungua kwa kutembea bila kupenda,” alisema Salum Juma wa Mbagala.
Naye John Katuvi alisema: “Huku ni kulazimishwa kufanya mazoezi, mimi nadhani serikali ifikirie upya uamuzi wa kuondoa kituo kile pale.“Ujue siyo wote tunaweza kushuka Makumbusho na kuchukua tena usafiri mwingine, ndiyo maana asubuhi utaona umati wa watu ukitembea, ukiwaona utadhani wanafanya mazoezi kwa kupenda kumbe hawana nauli ya kuunganisha magari.”

1 comment:

Anonymous said...

19:01





mwanaume gani wa namna hiyo kama umeshindwa mke rudisha kwao na muachane kwa amani ,mwanamke hapigwi namna hiyo,huyo binti ka angelikuwa ni dada yangu basi huyo sijui cha baba mngelimsahau kabisa ktk hii dunia.

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!