Tuesday, 16 September 2014

MENGI AINGIA FAINALI TUZO YA MFANYABIASHARA BORA AFRIKA

MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi ni miongoni mwa wafanyabiashara wanne waliofikia fainali ya kuwania Tuzo ya Mwaka ya Mfanyabiashara Bora Afrika (AABLA), kundi la Afrika Mashariki.


Sherehe za tuzo za AABLA, kundi la Afrika Mashariki zitafanyika Septemba 20 mjini Nairobi, Kenya na zitarushwa hewani na runinga barani Afrika.
Kwa mujibu wa chaneli ya runinga ya masuala ya fedha na biashara Afrika (CNBC Africa), ambao ndio waandaji wa sherehe hizo, tuzo hizo za kila mwaka zimebuniwa kwa ajili ya kutambua utendaji uliyotukuka katika biashara, wenye mafanikio makubwa kwenye sekta zao za biashara na vile vile kwenye jamii ambako biashara hizo zinaendeshwa.
“Tuzo hizo ni kutambua uongozi wa watu hao katika kubadilisha sekta ya biashara kwa kuendeleza ubora wa shughuli zao kwa kuzingatia desturi njema za kufanyabiashara na ubunifu,”.
“CNBC Africa, inajivunia kuendeleza utamaduni uliowekwa na tuzo hizi unaotambua na kusherekea mtazamo, msukumo wa mafanikio na ubora mkubwa wa viongozi wafanyabiashara katika bara la Afrika. AABLA inawatambua kipekee na kuwaheshimu viongozi ambao wamechangia katika kuboresha uchumi wa Afrika na waelekezi wa biashara zinazoongoza sasa,” ilisema taarifa hiyo kupitia tovuti : http://www.aabla2014.com.
Wafanyabiashara wengine watatu wateule wa tuzo hiyo ni Ofisa Mtendaji wa Britam, Benson Wairegi, Ofisa Mtendaji wa Centum, James Mworia, na Ofisa Mtendaji wa Crown Paints, Rakesh Rao (Kenya).
Watanzania wengine waliyoteuliwa katika tuzo hizo kwa makundi tofauti ni Ofisa Mtendaji wa Helvetic Solar Ltd, Patrick Ngowi, (EA Young Business Leader), na Ofisa Mtendaji wa Techno Brain Ltd, Manoj Shanker, (Entrepreneur of the Year).

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!