Tuesday 1 July 2014

TUSAIDIE KUPUNGUZA WATOTO WA MITAANI"

SERIKALI na taasisi za watu binafsi nchini, zimetakiwa kuongeza ushirikiano kwa kusaidiana na wazazi, ili kupunguza ongezeko la watoto yatima na wa mitaani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kupokea misaada ya vyakula na vinywaji kutoka kwa wahisani mbalimbali, Mlezi wa Kituo cha New Hope Family, Merry Stromberg, alisema kutokuwapo kwa ushirikiano  wa kutosha katika jamii na watu kujitolea, kunachangia kuongezeka tatizo hilo.
“Tunahitaji ushirikiano, wengi wanaliona hili tatizo lakini wanalifumbia macho. Watoto wa mitaani wanaonekana kuwa kero kwa jamii yetu, ukizingatia jinsi wanavyoomba na kuhangaika mitaani, si serikali wala wazazi suala tunaliona, kwanini tusijiunge kwa pamoja tulitokomeze?” alihoji.
Alielezea lengo la kuanzisha kwa kituo hicho ni kuhakikisha anajitolea kuwasaidia vijana wanaoteseka mitaani, hasa watoto wadogo wasiojua kujitegemea.
Alisema hadi sasa kituo kina watoto 45 wa jinsia zote kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, ikiwamo Morogoro, Singida, Iringa na Tabora.
“Tunachukua watoto wa kila aina ambao wanaishi maisha magumu, licha ya uwezo mdogo tulionao na changamoto zinazotukabili, kama watoto wanaosoma kukosa karo za shule na mavazi,” alisema.
Akizungumzia suala hilo kwa niaba ya wenzake baada ya kukabidhi msaada uliogharimu sh 700,000, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Namanga, Patricie Tungaraza, alisema inasikitisha kuona baadhi ya wazazi hawawafuatilii watoto wao na kuwaacha wakihangaika
TZ-DAIMA.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!