Pages
▼
Thursday, 24 July 2014
NI UKATILI GANI HUU? MAUAJI YA KUTISHA SINGIDA MWANAUME AWAKATAKATA MKE NA MTOTO KAMA NYAMA!
Tukio lingine la ajabu latokea Singida ambako mume amemkatakata au kamchinja mke wake na mtoto wake kama vile anachinja MNYAMA".
Hii fashion ya wanaume kuwaua wanawake kinyama imeshika ukanda sasa hivi karibu kila siku lazima kuwe na tukio kama hili kwakweli inasikitisha sana, kuona watu wamekuwa wanyama kiasi hiki, lakini nini hatima ya mauaji kama haya? Wanawake na watoto wanauawa bila hata sababu ya msingi, na hata kama kuna sababu za msingi huna madaraka ya kutoa roho ya kiumbe mwingine, vyombo husika vitoe adhabu kali kwa watu kama hawa, ili iwe fundisho kwa wengine, Sababu ya kuuawa kwa mama na mtoto haijajulikana, inasikitisha sana kuona wanaume wanamadaraka makubwa kiasi cha kuua kinyama kama hivi, serikali iangalie upya hili suala, wanaume wanatakiwa kuelimika kuwa kila mtu anahaki ya kuishi na kuwa na maamuzi yake mwenyewe, sio kuwa na mwanamke (mke) ni kuwa na madaraka yanayovuka mipaka, ambapo matokeo huwa ni kama haya
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA!
No comments:
Post a Comment