Monday, 14 July 2014

MTENVU AGAWA VYAKULA VYA SH MIL.6/-

Mtemvu agawa vyakula vya mil.6/-
MBUNGE wa Temeke, Abbas Mtemvu amegawa vyakula vyenye thamani ya sh milioni sita kwa vituo 15 vya kulea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu wilayani Temeke jijini Dar es Slaam.

Mtemvu alikabidhi mafuta ya kupikia ndoo 100; mchele mifuko 10; unga wa sembe mifuko 40; sukari kilo 20 na unga wa ngano mifuko 20 alipotembelewa na wawakilishi wa vituo hivyo ofisini kwake jana.
Alisema msaada huo ni utaratibu aliojiwekea tangu alipopata ubunge miaka nane iliyopita huku akisisitiza kwamba ni njia ya kuwajali wasiojiweza.
“Najua kuna watu wana uwezo wa fedha na vitu kama hivi lakini hawajui watazifikishaje kwa watu kama hawa, hivyo wanaweza kutupa wawakilishi kama sisi na tunawahakikishia tutavifikisha,” alisema Mtemvu.
Mwenyekiti wa Kituo cha Faraja Group kilichopo Kata ya Sandale, Suzan Kayange alisema msaada huo ni faraja tosha kwa watoto hao wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!