Pages

Wednesday, 23 July 2014

MANISPAA ZA JIJINI DAR-ES-SALAAM ZAJIIMARISHA KATIKA UKUSANYAJI WA KODI ZA MAJENGO

PICHA ZA KUKABIDHI VIFAA 3 - 1MAKALA: Na Rose Masaka-MAELEZO.

Kodi za majengo ni chanzo kikubwa kinachotegemewa na Halmashauri zote za Wilaya nchini zikiwemo Halmashauri za MkoaDar es Salaam ambazo ni Ilala,Kinondoni na Temeke.
Katika kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) hususani katika sekta ya fedha ili kuboresha ukusanyaji wa mapato ya Serikali kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo kodi ya majengo na kodi ya pango la Ardhi, mwaka 2013 Serikali iliona umuhimu wa kodi ya majengo ndipo ikachagua vyanzo hivi kuwa mfano katika kuleta ufanisi ili kutimiza malengo mbalimbali ya Halmashauri nchini na kuboresha mapato ya Serikali za Mitaa.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya alisema kuwa ukusanyaji wa kodi za Majengo umerudishwa kwenye Serikali za mitaa kwa maana ndiyo wanaojua nyumba zote, ambapo hapo awali kodi za majengo zilikuwa zikikusanywa na  Mamlaka ya Mapato (TRA),na baadaye Serikali iliona umuhimu wa Serikali za Mitaa kukusanya kodi hizi kwasababu wao ndiyo watu ambao wapo jirani sana na wananchi na wanafahamu nyumba zote ambazo zipo ndani ya mitaa yao.
Ili kufanikisha zoezi hili Halmashauri ziliona kuwa kuna umuhimu wa kuweka  malengo ambayo yatarahisha zoezi hili.
Kwa mujibu wa taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, matangazo kwenye vyombo vya habari na vipaza sauti ili kujenga uelewa kwa wananchi,pia kuorodhesha majengo yote kupitia watendaji wa kata na mitaa yaliweza kutolewa na Manispaa hiyo na kusambazwa kwenye vyombo vya habari nchini.
Waziri wa fedha, mhe. Saada Mkuya
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mwandisi Mussa Natty alisema kuwa Halmashauri yake ina wenyeviti wa mitaa wapatao 171na watendaji wa kata 34 ambao wanashiriki katika kufanya kazi ya kuainisha na kuorodhesha majengo kwa uthamini.
“Tumeweza kuyafanyia uthamini majengo 6,243 yenye thamani ya shilingi 1,493,360 na kodi inayotakiwa kukusanywa ni shilingi 2,538,712”. Alisema Mhandisi Natty.
Mhandisi. Natty ameongeza kuwa katika Manispaa yao wamefanya manunuzi ya vifaa vya ofisini ikiwemo magari kumi ili kurahisisha ufuatiliaji wa  mapato pia Halmashauri ya Kinondoni imefanikiwa kuanzisha mfumo wa malipo ya kielektroniki wa Maximalipo ambao umerahisisha malipo ya kodi katika maeneo ya karibu zaidi,kuondoa na kupunguza msongamano wakati wa malipo,kupata kumbukumbu za mlipa kodi kwa urahisi zaidi,uwazi na urahisi wa kufuatilia mapungufu.
Kwa upande wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyoBw. Photidas Kagimbo alisema kuwa wao wametoa mafunzo kuhusiana na uthamini kwa mkupuo kwa maafisa watendaji wa kata 30 na wenyeviti, pamoja na watendaji wa mitaa 180 wa Manispaa hiyo.
“Tumebaini jumla ya majengo 3,860 yenye thamani ya shilingi 145,652,498 na kiasi cha kodi ni shilingi 218,478. Alisema Bw. Kagimbo.
Aidha,Bw. Kagimbo amefafanua kuwa wamefanikiwa kuwapa watumishi uelewa wa matumizi ya TEHAMA katika utozaji wa kodi za majengo pia halmashauri imeagiza GPS Camera 5 zitakazozosaidia kuainisha ramani za majengo katika wilaya ya Temeke.

No comments:

Post a Comment